jeudi 21 novembre 2013

Kamati tendaji ya FFB mpya inaongozwa na Réverien NDIKURIYO tayari imeshakabiziwa ruhsa yakuanza kazi (Remise et reprise)

Pichani : Révérien NDIKURIYO na Lydia NSEKERA.

Ilikuwa ni jioni siku ya Jumaa-nne ndipo Révérien NDIKURIYO kiongozi mpya wa FFB alipewa wazifa wakuanza kutumika akiwa kama kiongozi wa shirikisho hilo pamoja na kundi lake linalo unda kamati tendaji . Tarehe 19 November 2013 ni tarehe ambayo haito sahaulika kwa upande wawapenzi wa mpira wa miguu na hususani kwa upande wa Shirikisho hilo .Kwenye ghafla hiyo mwanamama Lydia NSEKERA akishindikizwa na Mossi,Aboubakar walipishina na Jopo la kamati tendaji ya Révérien ambae siku hiyo alikuwa ameshindikizwa na Aimable alias Marandura,Hakizimana John, Moustafa Samugabo na Katibu mkuu Jéremie Manirakiza . 

Kiini chakupishana kwao madarakani ilikuwa kwa aliekuwa akiongoza FFB :
- Kutowa muhuli wa FFB (cachet),funguo za vyumba tofauti tofauti (clés des bureaux), nakuonyesha pesa zinazo saliya kwenye akaunti ya benk na kwenye sehemu yakuifadhiya vifaa vya Shirikisho hilo (présenter la situation bancaire au 18 novembre ainsi que celle des stocks de la fédération),na vile vile kutuma waraka kwa Interbank kusahihisha kuwa hana tena ruhsa ya muhuli kuhusikana kila swali linalo endana na pesa nawaraka huo aliumpa Kiongozi mpya wa FFB . (Ayant envoyé une lettre à l’Inter Bank Burundi pour signifier qu’elle n’a plus droit de signature des correspondances officielles, l’ex-présidente l’a remise à son successeur) . Alimkabizi vile vile waraka unao jiusisha nakuwakilishwa kwa Burundi kwwenye mashindano ya CHAN mwakani nchini South africa . Baada yakumaliza yote hayo Mwanamama Lydia Nsekera aliahidi kuweka bayana hesabu zote zinazo lingana na pesa zilizotumiwa kwa FFB na FIFA . Alizungumzia uoteshwaji wa nyasi zakisasa kwa upande wa uwanja wa ufundi (centre technique ) . Na kwenye upande wa ratiba zinazo endeleya kwa upande wa ushirikiano bora na nchi za nje , alisema kuwa nchi ya Japan iliahidi kutengeneza sehemu za mapumziko (vestiaires) na kujenga ukuta (clotures) kwa upande wa viwanja vya Kinama na Buyenzi . Aliweka bayana yale ambayoyalikuwa bado hayajatekelezwa ikiwa ni pamoja nakutolipa madeni ya Shirikisho kwa watumishi, Shirikisho za Mikoani ,akiahidi kuwa zote hizo ataziwakilisha kwenye ofisi hiyo ya FFb ifikapo siku ya Jumaa-mosi . Ifahamike ya kuwa waliohudhuriya mkutano huo waliona picha kinyume na ile ya wakati wauchaguzi kwani ilikuwa ni hali nzuri ya vichekesho,ilifkiya hadi mama Lydia Nsekera kumuombeya mmoja kati ya aliokuwa nawo kwenye uongozi wamshirikishe kwa wale watakao ishindikiza timu ya taifa , Aimable akamjibu nakusema kuwa ni swali watakalo fkiriya na jibu sahihi litatolewa . BB inawatakiya kwa mara nyingine Jopo mpya kuendesha vizuri FFB na kuileta sura mpya ya mabadiliko .
 
-Shukran za dhati vile vile kwa Tierry NIYUNGEKO kwa picha zake muruwa....

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire