dimanche 4 août 2013

Primusic 2013 : Washindi wa Mikoa ya Muyinga,Karuzi,Cankuzo,Ruyigi na Gitega.

Jury: Arnaud , Alida na Buddy Magloire

Mashindano ya Primusic 2013 yaliendelea kati kati na mwishoni wa hii wiki , Mikoa 5 ilipata fursa yakutembelewa na Washindi watakao wakilisha Mikoa hiyo kwa upande wa  ngazi ya Robo fainali ni pamoja na :

*Muyinga : Landry GATEKA na Landry GITARE

*Karuzi : NDUWAYO Melchiade na Clovis Arakaza

*Cankuzo : Jésus Marie Joseph Kavyinabuhiye hamwe na dada yake Clementine Divine Muhoza.


*Ruyigi : ARIANE KANYAMUNEZA na ALEXIS MUGISHA


*Gitega : Délos Nihorimbere , Mugisha Jean junior na yvannie Tunganirwa


Washindi hao walipatikana baada yakushindana mbele ya wachakachuaji maalum wa Primusic mwaka 2013 nao ikiwa ni pamoja na Buddy Magloire,Nganji Arnaud na Alida Baranyizigiye. Kwa upande wa Mikoa ya Muyinga , Karuzi , Cankuzo na Gitega walichakachuliwa na wanamemba wa Jury bila kuwepo Tamasha kwenye uwanja kama ilivyofanyika Bujumbura Vijijini , Ngozi , Kirundo , Ruyigi na hatimaye kufanyika mnamo saa chache leo Mkoani Muramvya .
10 wa Muramvya watakao pambana leo jioni.

Kwa upande wa Tamasha ya live ilio fanyika Mkoani Ruyigi , kama kawaida wasanii ambao ndio wabalozi mwaka huu wa mashindano hayo Sat B na Rally Joe walitimuwa vumbi hadi kuacha hoyi wapenzi wa mziki waliokuwepo kuja kushughudia moja kwa moja mashindano yenyewe. Mashindano hayo yalifanyika kwenye uwanja wa zamani wa Ruyigi . Leo hii ni zamu ya Mkoa wa Muramvya ambapo wasanii 10 tayari wameshatambulika watakao shindana saa nane mchana . Ni pamoja na :

Habonimana Gretta , Sinzinkayo Clovis Toussaint , Sebarundi Jelyusi , Nzojibwami Noé , Niyonkuru Olivier , Ntukamazina Venant , Ndayizeye Jerome , Nshimirimana Samuel , Ntakirutimana Anicet na Ndayizeye Emery.

# Mashindano hayo yataendelea ifwatavyo :

* Muramvya leo hii tarehe 4/August/2013

* Mwaro : Jumaa-tano tarehe  7/August/2013

* Rutana : Alkhamis tarehe 8/August/2013

*Makamba : Ijumaa tarehe 9/August/2013 ( Mkomboz atakuwepo kama mgeni rasmi ).

* Rumonge : Jumaa-pili tarehe 11/August/2013 ( Mkomboz atakuwepo tena kama mgeni rasmi )

* Bujumbura : Tarehe 13,14,15/August/2013 watachakachuliwa waimbaji mbele ya Jury (Auditions a huit clos ).

* Cibitoke : Ijumaa tarehe 16/August/2013

* Bubanza : Jumaa-mosi 17/August/2013

** Bujumbura : Jumaa-pili tarehe 18/August/2013 ,ndipo patakuwepo Tamasha yakutambuwa watakao wakilisha Mkoa wa Bujumbura . (T Max , mgeni rasmi kinyume na wabalozi Rally Joe & Sat b).


* Bujumbura : Robo fainali ( 1/4 final ) itakuwa Ijumaa tarehe 23/August na Jumaa-mosi 24/August/2013 .

* Gitega : Nusu fainali ( 1/2 final ) itakuwa tarehe 1/September/2013

* Bujumbura : Tarehe 8/September/2013 , patakuwa bonge la Tamasha lakuwatambulisha wasanii 6 watakao jishindia nakuingia kwenye fainali.Sehemu hapajatajwa ila itakuwa ni karibu ni fukwe la ziwa Tanganyika (Plage)

* Bujumbura : Fainali ya Primusic 2013 na Tamasha kubwa itakuwa terehe 14/September/2013 kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore .

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire