dimanche 17 mars 2013

Vital'o 0-0 Enougou Rangers , DC Motema Pembe 1-0 Lydia Ludic Burundi Academic


Saa tisa unusu ndipo mchuano wa duru ya awali kati ya timu ya Vital'o fc kutokea Burundi ambao walikuwa wenyeje waliridhika na sare ya tasa zidi ya timu kutokea Nigeria Enougou Rangers,mambano iliotizamwa na watu wasiokuwa wa dogo kwenye uwanja wa mwanamfalme Louis Rwagasore. Hatuna mengi yakuwafahamisheni kwani timu zote mbili zilicheza kwakuokopana,Vital'o ilizipata nafasi mbali mbali ila umaliziyaji ndio haukuwa mzuri . Kwa upande wa Lydia Ludic Burundi academic iliojielekeza nchini Jamuhuri yakidemokrasia ya Congo ilifungwa bao 1 kwa bila bao lililo patikana kwenye dakika ya 90',zikiwa zimesalia dakika chache mchuano huo umalizike. Kazi kwa timu zetu mbili ambazo ndizo balozi wa Burundi kwenye michuano hiyo yakimataifa ya Club zilizofanya vyema mwaka uliopita kwenye League zao . Marudiano ni mu wiki mbili.
Marefa walitokea nchini Lesotho
Waziri wa michezo na Lydia NSEKERA walikuwepo uwanjani.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire