mardi 11 février 2014

Hizi ni baadhi ya picha ya tokio la mvua kali iliyonyesha Mjini Bujumbura.

media

Jumaa-pili mida ya usiku ndipo mvua kali ilinyesha nchini Burundi  ,  maji mengi kutokea kwenye milima ilipituwa vitu na raia zaidi ya 50 . Tafara za kaskazini mwa Mjii mkuu wa Bujumbura ndizo zilikabiliyana na janga hilo . Mungu ainusuru Burundi... Izi ndizo picha za baadhi ya sehemu  tulizozipata :

Photo
Photo
Photo

Photo : Imvura yaguye mw'ijoro ryo kuruyu w'imana yarahitanye abantu batari bake n'ibintu mu buraruko bw'igisagaraca Bujumbura. Ibitigiri mfatakibanza vyabitavye Imana muri commune  Kamenge n'abantu 96. Isoko yo mu Kamenge yarabomotse eka n'amazu atari make yanabomotse.
Reta muntumbero yo gufasha, yafashe ingingo zimwe zimwe, abitavye Imana niyo  ibahambisha, abakomeretse nabo bariko baravugwa k'ubuntu mubitaro vya Reta.

vendredi 7 février 2014

Nyimbo mpya ya Big Farious *what's my name * feat Chany Queen iko tayari ,soma mistari aliyo imba kwenye pini hiyo...

Leo hii usiku mida ya saa mbili ndipo MUGANI DESIRE a.k.a Big Fizzo ameiweka hadharani nyimbo yake mpya *Whats my name * featuring CHANY QUEEN aliyo rikodia Technolojia sounds pamoja nae Docta Jack na A Tizo . Tukiwa tunamuhoji kuhusikana na pini hiyo ambayo ina ujumbe mzito mno alitujibu mengi nakutufahamisha mengi kuhuskina na ratiba ya Tamasha na mengineyo :
Pichani : Fizzo pamoja na Sony Kabu Cherche kabu trouve...

Fizzo :" Nimeamuwa kuichia hadharani pini yangu mpya niliyomshirikisha Chany Queen , zipo nyimbo 3 kuna * best friends , Yahaya na Whats my name najuwa ni nyimbo itakayo wa touch wengi , mimi kama msanii kimbilio langu ni mziki , ninapokuwa na raha ao karaha , kulikuwepo maneneo mengi na hadi mdaa huu yapo , nimetupa jiwe gizani,sijamlenga mtu yule litakalo mgusa basi kimpango wake . Sijatangaza bifu na mtu , najiamini kivyangu ,mimi najisifu nikisema nimeanza kitambo,kwenye game hili nimeanza kitambo , eshima ni kitu cha lazima na chabure . Inakuwa siyo vizuri japo una pesa ,dawa ya ubisho ni kuwa bisho zaidi . Baada ya hii apa ntatengeneza nyingine inakayo julikana kwa jina la * JAJA* , hii apa ni kama whats my name namba 2 ila yenyewe nitakuwa namuenzi Mzee wangu ambae kisha tutoka kitambo , nikama namuenzi vile namfahamisha maswali magumu ambayo yamenikabili kwa mdaa huu . Kuhusu beef nawaweka watu ulimwengu kuwa sina beef na yeyote ,wengi wanazungumzakuhusu lolilo na Franck Duniano ,kiukweli sijuwi nini kwa upande wa hawa wawili . Natangaza live , Lolilo kama nimewahi kukukoseya naomba samahani  , Franck ni rapa mzuri tena anaweza , na kama tulikuweka kwenye Kundi la Wanajeshi ni kwakuwa unaweza ,endelea kazi yako ,nilikuwa nakuamini na bado kwasasa nakuamini ,kama unahitaji kutoka kwenye kundi ni ruhsa yako ,usitaki kutoka kwa beef , nakusihi uendeleye na uko na ruhsa yakutoka na wende unapotaka . Kuhusu Wanajeshi ni kuwa tuko busy sana kila mtu anafanya za kwake ,wakae mkao wa kula ivi karibuni tutafanya mambo makubwa . Tarehe 8/February/2014 niko na Show Rumonge pamoja nae T Max . Tarehe 14 February siku ya wapendanao ntakuwa Archipel pamoja na wanangu Sat B , Black G , na Franck g80 . Vile vile watu wa Dubai mjiandae hapo tarehe 15/February/2014 . Lakufahamu lingine ni kuwa FIZZO ni mmoja kati ya Wasanii ambao wamepewa shavu na Kampuni ya IKOH Multiservice , amepewa shavu ya nyimbo ambayo imeingia tayari kwenye compilation ya Volume 1 ya YOU'LL LOVE CHANGE'S . Jana ndipo alikuwa studio na tayari kurikodi pini hiyo chini ya ufundi wa BOTCHUM ."

Ukitaka kuskiliza fool interview niliyofanya na Big Farious jiunge na link hii : www.radioburundibwiza.com

jeudi 6 février 2014

South africa : Tizama video mpya ya Bujumbura ndio nyumbani by S.U ft Dogo redHii ndio video tuliokuwa tunaisubiri kwa hamu , ni wasanii wawili kutoka Burundi, mmoja anaitwa S.U mungine Dogo Red . Iyo ni kazi yao, enjoy it...

Usikose kujiunga na Buja Extreme Party week end hii...

Siku ya Ijumaa na Jumaa-mosi  tarehe 7 na 8 February 2014 kwenye ukumbi wa Panoramique (Celexon Hotel ) , barabara ya JRR Mjini kati ndipo patafanyika Tamasha mbili za uanzilishi wa Club mpya (Boite de Nuit )  . Ifikapo Ijumaa pameandaliwa Tamasha ya Buja Surprise Friday Party , Jumaa-mosi itakuwa Saturday Night Live ambapo Dj kutoka nchini Kenya anae julikana kwa jina la DJ PIERRA pichani kwenye bango  , DJ T.T kutoka Kampala Uganda na DJ Noah kutoka Burundi watakonga nyoyo za Washabiki watakao jumuika kwenye usiku huo . Duru kutoka kwa DAN mmoja kati ya walio anda ujio huo na kuweka mazingira sawa ametufahamisha kuwa :'' Kila kitu kiko sawa , na tunaomba watu wafike kwa wingi kutupa sapoti , tunaimani kuwa mazingira yatakuwa mazuri .''

mercredi 5 février 2014

Matokeo ya Wiki ya 8 Ligi ya taifa nchini Burundi (Vital'o Fc 0-0 Inter star ,LLB 1-2 Athletico ...)


Hapo jana tarehe 4/2/2014 kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore sawa na viwanja vingine vya soka ilichezwa michuano ya wiki ya 8 ya Ligi ya taifa . Mchuano uliyokuwa unasubiri kwa hamu ni ule uliyo zipambanisha Timu pinzani . Mchuano kati ya timu hizo mbili uliwakusanya Washabiki wengi , wapenzi na wadau wa soka , hali ambayo siku nyingi ilikuwa haishughudiwi nchini . Vital'o Fc ambayo iliwapoteza Wachezaji wasiokuwa wadogo baadhi yao wakiwa wameuzikana nje ya nchi na wengine wakiwa wamejiunga na mpinzani wao Inter Star nikizungumzia wachezaji kama DEO NDAYISHIMIYE , NKURIKIYE LEOPOLD KAYA , MICHEL GIRUKWISHAKA na NKURUNZIZA D'AMOUR , kinyume na hao wa Vital'o Fc timu ya Inter star inayo ongozwa na Mh mbunge wa Rumonge KARENGA RAMADHAN imejizatiti vile vile wachezaji kama CHENE MOHSIN , POUTCHOU DEGUERRE , NDUWIMANA SAIDI TAMAA . Kwa upande wa Vital'o Fc kinyume na MIAMI MBAKIYE BABY , JOHN GIRUKWISHAKA , IDDY DJUMAPILI , ABDALLAH MASSOUD , wengi wao ni wapya nikizungumzia kama Wachezaji wa 3 MOUSSA MOSSI HADJ , Kipa OMAR ,na Ballack kutoka kwenye Klabu ya Flambeau de l'Est , Muyaga kutoka kwenye Academie tchite , Zola kutoka Inter star  ndio walijiunga na Klabu hiyo mwaka huu . Fahamu ya kuwa mchuano wao ulimalizika kwa sare ya tasa yakutofungana 0-0 , na Vital'o Fc imesalia kwenye kileleni...

Haya ndio matokeo ya Wiki ya 8 ligi ya Taifa :
---------------------------------------------------------------

Vital’O FC - Inter Stars / Prince Louis Rwagasore , saa Kumi ( 16h ).

LLB Academic 1-2 Athletico Olympic / Prince Louis Rwagasore , saa nane ( 14h ).

Flamengo FC 1-1Royal FC / Buterere ,saa nane ( 14h ).

Muzinga FC 1-1 Volontaires FC / Buterere ,saa Kumi ( 16h ).

Le Messager Ngozi 2-1 Espoir FC / Gatumba ,saa kumi ( 15h ).

Fahamu vile vile ya kuwa Flambeau de l'Est na Academie Tchite hazikucheza kulingana na maandalizi ya kombe la Klabu bingwa flambeau de l'Est yaweza kusafiri Jumaa-tano hii kuelekea Congo-Brazzaville na Academie Tchite safari yake ikiwa imepangwa hapo kesho alkhamis ambao wao wataelekea nchini Rwanda kumenyana na AS KIGALI ya Rwanda . 

Tukizungumzia kandanda nchini uingereza ni  kuwa Mkufunzi Laudrup wa Swansea alifutwa kazi na  klabu hiyo ,taarifa hizo zinajiri siku moja tu baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo Huw Jenkins kupuuzilia mbali tetesi kuwa walikuwa wamezungumzia mustakabali wa Laudrup. Uvumi ulikuwa umesambaa kuhusu hatma ya Laudrup baada ya Swansea kushindwa kwa mabao 2-0 dhidi ya West Ham Jumamosi iliyopita.

Hiyo ilikuwa mara ya sita timu hiyo kupoteza katika mechi nane za Ligii kuu ya Uingereza na kuiacha na alama mbili tu juu ya timu ambazo zitateremshwa katika ligii hiyo.

Monk alikuwa amepigiwa debe kuchukua nafasi hiyo ikiwa mojawapo ya njia za kuboresha kikosi hicho.                                                 


dimanche 2 février 2014

MATOKEO YA LIGI A : Vital'o Fc 1-0 Muzinga ,Inter Star 3-1 Athletico , LLB Ac. 0-0 Espoir Gatumba...

Ligi ya taifa ,daraja la kwanza jana tarehe 1/2/2014 na leo tarehe 2/2/2014 kwenye Viwanja tofauti nchini :

Matokeo ya week-end :

Royal FC 2-0 Prince Louis FC /  Muramvya

Le Messager Ngozi 4-0 Volontaires / Ngozi

Espoir FC 0-0 Lydia Ludic Burundi /  Gatumba

Vital'O FC  1  -  0 Muzinga FC /  Bujumbura
( Miami 73')
Flamengo FC 0-1 Académie Tchité /  Buterere

Inter Stars            3      -   1 Athletico Olympic /  Bujumbura
 (Kaya 20' , Deo 27' , Shassir 92')  - (Aimée Nzohabonayo 85')

Jumaa-pili tarehe 2/2/2014 Bujumbura

Flambeau de l'Est 1-0 Guepiers du Lac .

Msimamo wa muda wiki ya 5 :
---------------------------------------

Equipes
GB
Points
   1.
Vital'o
6
12

   2.
Flambeau
4
11

   3.
LydiaLudic 
5
9

   4.
Messager 
4
9

   5.
Inter star
3
9

   6.
Prince  louis39

   7.
Académie
. Tchite 
1
9

   8.
Guêpiers
 du Lac
4
8

   9.
Volontaire
-6
8

   10.
Royal
-2
7

   11.
Muzinga
-3
6

   12.
Espoir-5
3

   13.
Athletico Olympic
-4
2

   14.
Flamengo
-5
2


TAMBWE AMISSI ni mmoja kati ya wanaongoza safu ya wafumania nyavu nchini Tanzania + habari za usajili uingereza

MSHAMBULIAJI Mrundi Amisi Tambwe wa Simba amesema hakutegemea kufunga mabao matatu peke yake 'hat-trick' katika mchezo wao wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara waliopata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya 'maafande'a Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba imefufua ndoto zake za kufanya vizuri msimu huu baada ya kuwashindilia mabao hayo maafande hao wanaonolewa na kocha mpya, Hemed Morocco, ambaye mzunguko wa kwanza alikuwa akikifua kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara 1988, Coastal Union. Shukrani kwa mabao ya kiungo Jonas Mkude dakika ya 10 na Tambwe dakika za 22, 28 na 50. Akizungumza na BIN ZUBEIRY mara tu baada ya kukabidhiwa mpira wake kwa kukipa hat-trick na refa Nathan Lazaro kutoka Kilimanjaro, Tambwe aliyeonekana mwenye furaha tele, alisema hakutarajia kuona timu yake ikiibuka na ushindi huo mnono kwa vile maafande hao wana timu ngumu kuruhusu nyavu zake kuitikishwa.
"Kwa kweli sikutegemea kufunga hat-trick katika mechi ya leo, unajua hawa jamaa (Oljoro JKT) wana timu nzuri ambayo si rahisi kufungika. Tulicheza nao Arusha tyukawafunga goli moja tu nami sikufunga, nakumbuka walipata penalti siku hiyo (Agosti 28 mwaka jana) lakini bahati mbaya wakakosa," amesema Tambwe.
"Sijui wamejisahau vipi leo ... sikutarajia kufunga hat-trick kabisa ndiyo maana nimeshangilia sana baada ya kufunga bao la nne kwa timu yangu. Nafikiri kujituma kwanga na timu kwa ujumla mazoezini ndiko kumetufikisha hapa.
"Unajua nafanya mazoezi kwa nguvu na nafunga sana mazoezini, natumaini nitafanya vizuri zaidi katika michezo inayofuata ili kuisaidia timu kupata mafanikio," amefafanua zaidi Tambwe, ambaye baada ya kukamilisha hat-trick yake amenaswa na kamera za BIN ZUBEIRY akirukaruka kushangilia.
Hat-trick hiyo pengine imemwondolea ngundu nyota huyo ambaye alikuwa hajafunga goli hata moja katika michezo nane aliyokichezea kikosi cha Kocha Mcoaratia Zdravko Logarusic tangu afunge mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga katika mchezo wa 'Nani Mtani Jembe' uliopigwa Uwanja wa Taifa Desemba 21 mwaka jana.
Baada ya mchezo huo uliofukuizisha benchi zima la ufundi la Yanga lililokuwa linaongozwa na Mholanzi Ernie Brandts, Simba ilicheza mechi nane: sita za mashindano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzabar, moja ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar waliyofungwa 1-0 na moja ya ligi dhidi ya Rhino Rangers wakishinda 1-0 lakini mkali huyo wa kufumania nyavu -- Tambwe alikuwa hajapachika hata bao moja.
Mabao matatu ya jana, yamemfanya Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Kombe la Kagame mwaka jana, kufikisha idadi ya mabao 13 katika ligi hiyo msimu huu, matatu mbele ya mfungaji bora wa msimu uliopita, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast.
Kabla ya mechi ya jana, Tchetche aliyefunga mabao yote mawili katika ushindi mwembamba wa 1-0 ambao Azam FC imeupata katika mechi mbili mfululizo za mzunguko wa pili dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara 1999 na 2000, Mtibwa Sugar Januari 25 na Rhino Rangers Jumatano, alikuwa na mabao 10 sawa na Tambwe.
Ushindi huo unaifanya Simba iliyopata ushindi katika mechi mbili mfululizo za mzunguko wa pili ifikikshe pointi 30 baada ya kucheza mechi 15 katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi, pointi moja nyuma ya wababe Mbeya City, mbili nyuma ya Yanga na tatu Azam FC walioko kileleni.
Kabla ya kujiunga na Simba msimu huu akitokea Klabu ya Vital'O ya Burundi aliyoipa ubingwa wa Kombe la Kagame mwaka jana nchini Sudan, Tambwe alikuwa ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Burundi.
Mabao ya Tambwe na Mkude ya leo yanafanya idadi ya mabao kufikia 230 kwani kabla ya mechi mbili za leo, idadi ya mabao ilikuwa 224. Wachezaji wawili wa Mgambo Shooting, Peter Mwalianzi na Bolly Shaibu pia wamefunga bap moja kila mmoja katika ushindi wa 2-0 ambao timu yao imeupata dhidi ya 'Wauza Mitumba wa Ilala' Ashanti United kwenye Uwanja wa Azam (Azam Complex) jijini leo jioni.
Mzunguko wa kwanza yalifungwa mabao 208 huku mshambuliaji bora wa Kombe la Kagame mwaka jana, huku Tambwe akifunga mabao 10 na kuongoza safu ya wafumania nyavu mzunguko wa kwanza.
Mshambuliaji wa Coastal ambaye hakufunga hata bao moja mzunguko wa kwanza, Mganda Lutimba Yayo ndiye mchezaji wa kwanza kufunga bao mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo akiifungia timu yake bao la dakika ya nne tu ya mchezo wao wa kwanza waliolazimishwa sare ya bao moja na maafande wa OPljoro JKT nyumbani kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Januari 25.
Aidha, hakuna mchezaji aliyefunga bao kwa njia ya penalti mzunguko wa pili ambao mpaka sasa penalti moja tu imeshatolewa kwa Simba katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Rhino walioshinda 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili. Kiungo aliye katika kiwango cha juu cha soka, Ramadhani Singano 'Messi' licha ya kuuifungia Simba bao hilo la ushindi alikosa penalti hiyo. Mpigaji wa penalti wa Simba kwa sasa,
Tambwe alikuwa ametolewa na kocha Logarusic wakati tuta hilo likitolewa. Katika mabao yake 10, Tambwe amefunga mabao matatu kwa njia ya penalti. Jerry Santo ndiye anaoongoza kwa kuwa na mabao mengi zaidi ya penalti. Mkenya huyo aliifungia Coastal mabao manne kwa njia hiyo mzunguko wa kwanza.
Jumla ya penalti 25 zimeshatolewa na marefa wa ligi hiyo msimu huu, 24 zikiwa ni za mzunguko wa kwanza. Penalti zilizofungwa ni 20 huku wachezaji wanne wakiungana na Messi kwa kukosa penalti mzunguko wa kwanza. Wachezaji hao ni Stanley Nkomola (JKT), Babu Ally (Oljoro), Elius Maguri (Ruvu) na Jeremiah Juma (Prisons).
Winga hatari wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars), Mrisho Ngassa, ndiye mchezaji anayeonekana kuwa hatari zaidi na pengine ndiye mchezaji bora wa ligi hiyo kwa takwimu zilizopo. Katika michezo saba ya mzunguko wa kwanza ambayo mchezaji huyo wa zamani wa Kahama United, Kagera Sugar, Azam FC na Simba aliichezea Yanga, alifunga mabao sita na kupika mabao mengine sita.
Mzaliwa huyo wa Mwanza, hakucheza michezo mitano ya mwanzo kutumikia adhabu ya kukosa mechi sita aliyopewa na Shirikisho la Soka (TFF) baada kubainika kuwa alijisajili katika klabu mbili za Simba na Yanga kuzitumikia msimu huu. 

USAJILI WAFUNGWA ULAYA TAREHE 31/1/2014, WALIOINGIA NA KUTOKA KLABU ZOTE 
ZA LIGI KUU ENLGAND SOMA HAPA :------------------------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------

- PAZIA la usajili wa dirisha dogo Ulaya limefungwa usiku wa Tarehe 31/1/2014 na ifuatayo ni taarifa ya usajili wa klabu zote za England, wachezaji waliotemwa na kusajiliwa.

ARSENAL: Imesajili mchezaji mmoja tu, Kim Kallstrom kwa mkopo kutoka Spartak Moscow, wakati walioondoka ni Chuba Akpom (Brentford, mkopo), Anthony Jeffrey (Wycombe, mkopo), Benik Afobe (Sheffield Wednesday, mkopo), Nico Yennaris (Brentford) Emmanuel Frimpong (Barnsley), Daniel Boateng (Hibernian, mkopo), Park Chu-Young (Watford, mkopo).

ASTON VILLA: Waliosajiliwa ni Grant Holt (Wigan, mkopo) na Ryan Bertrand (Chelsea, mkopo), wakati walioondoka ni Stephen Ireland (Stoke), Michael Drennen (Carlisle, mkopo) na Jordan Graham (Bradford, mkopo).

CARDIFF: Waliosajiliwa ni Magnus Wolff Eikrem (Heerenveen, Pauni Milioni 2), Mats Moller Daehli (Molde), Jo Inge Berget (Molde), Kenwyne Jones (Stoke, kubadilishana), Fabio da Silva (Manchester United), Wilfried Zaha (Manchester United, mkopo). Walioondoka ni Rudy Gestede (Blackburn), Filip Kiss (Ross County, mkopo), Nicky Maynard (Wigan, mkopo), John Brayford (Sheffield Utd, mkopo), Peter Odemwingie (Stoke, kubadilishana), Simon Moore (Bristol City, mkopo), Craig Conway (Blackburn Rovers, mkopo) na Andreas Cornelius (FC Copenhagen).

CHELSEA: Waliosajiliwa ni Bertrand Traore (Association Jeunes Espoirs De Bobo-Dioulasso), Nemanja Matic (Benfica, Pauni Milioni 21), Mohamed Salah (Basel Pauni Milioni 11) na Kurt Zouma (Saint Etienne, Pauni Milioni 12.5), wakati walioondoka ni Bertrand Traore (Vitesse Arnhem, mkopo), Kevin de Bruyne (Wolfsburg, Pauni Milioni 17), Ryan Bertrand (Aston Villa, mkopo) Josh McEachran (Wigan, mkopo), Juan Mata (Manchester United, Pauni Milioni 37.1) Michael Essien (AC Milan), Sam Walker (Colchester, mkopo), Nathaniel Chalobah (MIddlesbrough, mkopo), Kenneth Omeruo (Middlesbrough, mkopo), Patrick Bamford (Derby, mkopo) na Gael Kakuta (Lazio, mkopo).

CRYSTAL PALACE: Waliosajiliwa ni Jason Puncheon (Southampton), Scott Dann (Blackburn), Wayne Hennessey (Wolves, Pauni Milioni 3), Tom Ince (Blackpool, mkopo) na Joe Ledley (Celtic), wakati walioondoka ni Jason Banton (Plymouth, huru), Jimmy Kebe (Leeds, mkopo), Kwesi Appiah (Notts County, mkopo), Matt Parsons (Plymouth), Jack Hunt (Barnsley, mkopo) na Jose Campana (Nuremburg, mkopo).

EVERTON: Waliosajiliwa ni Aiden McGeady (Spartak Moscow), Lacina Traore (Monaco, mkopo) na Jindrich Stanek (Sparta Prague) wakati walioondoka ni Nikica Jelavic (Hull), Matthew Kennedy (Tranmere, mkopo), Shane Duffy (Yeovil, mkopo), Hallam Hope (Northampton, mkopo), Chris Long (MK Dons, mkopo), Matthew Pennington (Tranmere, mkopo) na Johnny Heitinga (Fulham, huru).

FULHAM: Waliosajiliwa ni Clint Dempsey (Seattle Sounders, mkopo), William Kvist (mkopo, Stuttgart), Lewis Holtby (Tottenham, mkopo), Konstantinos Mitroglou (Olympiacos, Pauni Milioni 12.4) na Johnny Heitinga (Everton, huru), wakati walioondoka ni Bryan Ruiz (PSV, mkopo), Stephen Arthurworrey (Tranmere, mkopo), Marcus Bettinelli (Accrington, mkopo), Jack Grimmer (Port Vale, mkopo), Aaron Hughes (QPR, undisclosed), Dimitar Berbatov (Monaco, mkopo).

HULL: Waliosajiliwa ni Nikica Jelavic (Everton), Elliott Kebbie (Atletico Madrid, mkopo), Shane Long (West Brom, Pauni Milioni 6), wakati walioondoka ni Tom Cairney (Blackburn, Pauni 500,000), Conor Townsend (Carlisle, mkopo), Eldin Jakupovic (Leyton Orient, mkopo), Cameron Stewart (Leeds, mkopo), Nick Proschwitz (Barnsley, mkopo), Gedo (Al Ahly) na Aaron Mclean (Bradford).

LIVERPOOL: Hakuna aliyesajiliwa, wakati walioondoka ni Adam Morgan (Yeovil, huru), Tiago Ilori (Granada, mkopo), Craig Roddan (Accrington Stanley, mkopo), Ryan McLaughlin (Barnsley, mkopo) na Michael Ngoo (Walsall, mkopo).

MANCHESTER CITY: Hakuna aliyesajiliwa wakati walioondoka ni John Guidetti (Stoke, mkopo), Albert Rusnak (Birmingham mkopo), Emyr Huws (Birmingham, mkopo) na Abdisalam Ibrahim (ametemwa).

   * Usajili uliogharimu fedha nyingi zaidi dirisha hili dogo niwa Juan Mata.

MANCHESTER UNITED; Aliyesajiliwa ni Juan Mata pekee kutoka Chelsea kwa Pauni Milioni 37.1), wakati walioondoka ni Jack Barmby (Hartlepool, mkopo), Anderson (Fiorentina), Fabio da Silva (Manchester United), Wilfried Zaha (Cardiff, mkopo), Fabio da Silva (Cardiff), Tom Lawrence (Yeovil Town, mkopo), Tyler Blackett (Birmingham City, mkopo), Sam Byrne (Carlisle United, mkopo), Charni Ekangamene (Carlisle United, mkopo), Tom Thorpe (Birmingham City, mkopo), Federico Macheda (Birmingham City, mkopo), Will Keane (QPR, mkopo) na San Johnstone (Doncaster Rovers, mkopo).

NEWCASTLE; Aliyesajiliwa ni Luuk de Jong (Borussia Monchengladbach, mkopo) pekee, wakati walioondoka ni Yohan Cabaye (Paris-Saint Germain, Pauni Milioni 23), Jonas Gutierrez (Norwich, mkopo), Curtis Good (Dundee United, mkopo).

NORWICH; Imemsajili Jonas Gutierrez pekee kwa mkopo kutoka Newcastle, wakati walioondoka ni Daniel Ayala (Middlesbrough, Pauni 350,000) na Jamar Loza (Leyton Orient, mkopo).

SOUTHAMPTON; Hakuna aliyesajiliwa wakati walioondoka ni Lee Barnard (Southend, mkopo), Danny Fox (Nottingham Forest, mkopo), Billy Sharp (Doncaster, mkopo), Dani Osvaldo (Juventus, mkopo), Jason Puncheon (Crystal Palace).

STOKE; Waliosajiliwa ni John Guidetti (Man City, mkopo), Stephen Ireland (Aston Villa), Juan Agudelo (New England Revolution), wakati walioondoka ni Brek Shea (Barnsley, mkopo), Jamie Ness (Leyton Orient, mkopo) na Juan Agudelo (FC Utrecht, mkopo).

SUNDERLAND; Waliosajiliwa ni Marcos Alonso (Fiorentina, mkopo), Santiago Vergini (Estudiantes, mkopo), Oscar Ustari (Almeria), Ignacio Scocco (Internacional, Pauni Milioni 3), Liam Bridcutt (Brighton, Pauni Milioni 2.5), wakati walioondoka ni Mikael Mandron (Fleetwood, mkopo), Ji Dong-won (Augsburg), Billy Knot (Port Vale, mkopo), Cabral (Genoa, mkopo), Modibo Diakite (Fiorentina, mkopo), David Moberg Karlsson (Kilmarnock, mkopo), David Vaughan (Nottingham Forest, mkopo) na Duncan Watmore (Hibernian, mkopo).

SWANSEA; Waliosajiliwa ni David Ngog (Bolton), Raheem Hanley (Blackburn), Jay Fulton (Falkirk) na Marvin Emnes (Middlesbrough, mkopo), wakati walioondoka ni Alan Tate (Aberdeen, mkopo), Daniel Alfei (Portsmouth, mkopo), Rory Donnelly (Coventry City, mkopo)

TOTTENHAM; Hakuna aliyesajiliwa wakati walioondoka ni Jermain Defoe (Toronto, Pauni Milioni 6), Simon Dawkins (Derby), Shaquile Coulthirst (Leyton Orient, mkopo), Jon Obika (Brighton, mkopo), Ryan Fredericks (Millwall, mkopo), Adam Smith (Bournemouth), Lewis Holtby (Fulham, mkopo).

WEST BROMWICH ALBION; Aliyesajiliwa ni Thievy Bifouma pekee kutoka Espanyol kwa mkopo,wakati walioondoka Lee Camp (Bournemouth), Shane Long (Hull, Pauni Milioni 6), George Thorne (Derby, mkopo).

WEST HAM: Waliosajiliwa ni Roger Johnson (Wolves, mkopo), Antonio Nocerino (Milan), Marco Borrielo (Roma, mkopo) Abdul Razak (Anzhi Makhachkala), Pablo Armero (Napoli, mkopo), wakati waliosajiliwa ni Blair Turgott (Rotherham, mkopo), Jordan Spence (MK Dons, mkopo), Paul McCallum (Hearts, mkopo) na Modibo Maiga (QPR, mkopo).

100.000Euros ndizo pesa alizonunuliwa YAMIN kuelekea FC TIRANA ya Albania...

Hii ndio orodha ya Wachezaji wa FC TIRANA msimo wa 2013 - 2014 . Fahamu ya kuwa YAMIN SELEMANI NDIKUMANA mwenye umri wa miaka 26 amesajiliwa na ndonge nono la pesa , Yuro 100.000 (100.000Euros) , pesa nyingi kwa mchezaji kutoka kwenye nchi kama Burundi , hali hiyo kutokea ni mara chache sana. Kwa upande mungine fahamu ya kuwa Fiston Abdul Razzak kwasasa yupo nchini Kenya kwenye mazungumzo ,halakuli hali hali itakavyokuwa itakuwa vigumu kucheza Lii ya nyumbani kwani kuna duru za ndani tulizopata zinazo sema kuwa ikiwa bitashindikana Kenya , aweza akajielekeza nchini South africa , kingine ni kuwa mchezaji NSABIYUMVA Frederick ya kwake yamekwisha , ifikapo kesho Jumaa tatu tarehe 3/2/2013 aweza kujiunga na Jomo Cosmos / South africa.
Hii ndio orodha ya Wachezaji 32 wa Fc Tirana . Raia wa Albania ni 28 , 4 pekee ni kutoka nje ya nchi yao :

#Name / PositionnationMarket value
-
Ilion LikaLika, Ilion
Goalkeeper (GK), 33 Years
 125.000 £
150.000 €
-
Xhino SejdoSejdo, Xhino
Goalkeeper (GK), 22 Years
 25.000 £
25.000 €
-
Marsel CakaCaka, Marsel
Goalkeeper (GK), 18 Years
 100.000 £
125.000 €
-
Endri SaraciSaraci, Endri 2
Goalkeeper (GK), 18 Years
 -
-
Erjon BrakaBraka, Erjon
Defence , 18 Years
 -
-
Gentjan MucaMuca, Gentjan
Defence (CB), 26 Years
 100.000 £
100.000 €
-
Entonjo PashajPashaj, Entonjo
Defence (CB), 29 Years
 100.000 £
125.000 €
-
Ardit PeposhiPeposhi, Ardit
Defence (CB), 20 Years
 50.000 £
50.000 €
-
Ervis KajaKaja, Ervis
Defence (CB), 26 Years
 100.000 £
100.000 €
-
Blerim KotobelliKotobelli, Blerim
Defence (LB), 21 Years
 50.000 £
50.000 €
-
Erion HoxhallariHoxhallari, Erion
Defence (LB), 18 Years
 75.000 £
75.000 €
-
Endri VrapiVrapi, Endri
Defence (LB), 31 Years
 100.000 £
100.000 €
-
Reinaldo KalariKalari, Reinaldo
Defence (LB), 29 Years
 75.000 £
75.000 €
-
Elvis SinaSina, Elvis
Defence (RB) -, 35 Years
 100.000 £
100.000 €
-
Mateos CakeCake, Mateos 2
Midfield , 18 Years
 25.000 £
25.000 €
-
Afrim TakuTaku, Afrim
Midfield (DM), 24 Years
 150.000 £
175.000 €
-
Erando KarabeciKarabeci, Erando
Midfield (CM), 25 Years
 250.000 £
275.000 €
-
Erlind KoreshiKoreshi, Erlind
Midfield (RM), 26 Years
 75.000 £
75.000 €
-
Dorian KerçikuKerçiku, Dorian
Midfield (RM), 20 Years
 100.000 £
100.000 €
-
Ivan DelicDelic, Ivan
Midfield (AM), 27 Years
 250.000 £
275.000 €
-
Mensur LimaniLimani, Mensur
Midfield (AM), 29 Years
 75.000 £
75.000 €
-
Francis KahataKahata, Francis
Midfield (LW), 22 Years
 -
-
Gilberto FortunatoFortunato, Gilberto
Striker , 26 Years
 -
-
Hanc LlagamiLlagami, Hanc 2
Striker , 18 Years
 25.000 £
25.000 €
-
Mirel CotaCota, Mirel
Striker (SS), 25 Years
 150.000 £
175.000 €
-
Selemani NdikumanaNdikumana, Selemani
Striker (CF), 26 Years
 100.000 £
100.000 €
-
Mario MorinaMorina, Mario
Striker (CF), 21 Years
 175.000 £
200.000 €
-
Ergys SorraSorra, Ergys
Striker (CF), 24 Years
 50.000 £
50.000 €
Total value 2.300.000 £
2.625.000 €
28 Players, thereof 4 Foreign players (14,3 %)

Mengi zaidi ,tizama hapa : http://www.transfermarkt.co.uk