vendredi 17 janvier 2014

Huyu Mchezaji Ndio Kocha Mpya Wa AC Milan


Baada ya miaka 22 uwanjani akicheza game kali sana la soka Nyota mkongwe wa AC Milan Clarence Seedorf ametangaza rasmi kustaafu kucheza mpira wa miguu ili aweze kuchukua nafasi ya ukocha ndani ya San Siro.

Seedorf amekuwa akihusishwa sana na nafasi ya ukocha tangu kuanza kwa msimu wakati Milan ikiwa taabani kiubora na matokeo chini ya Massimiliano Allegri.

Allegri aliondolewa kazini kufuatia kichapo cha mshituko cha mabao 4-3 kutoka kwa Sassuolo mwishoni mwa wiki, na kuongeza minong'ono kuwa Seedorf alikuwa akitayarishwa kuchukua nafasi hiyo kwa kigogo hicho cha Serie A ambapo mkongwe huyo wa kimataifa wa Uholanzi amethibitisha hii leo kuwa mpango huo umekwenda vizuri kabla ya kuchukua nafasi hiyo.

Akiwa na umri wa miaka 2I, Seedorf alikaririwa akisema kuwa atastaafu kucheza soka atakapo kamilisha miaka 22 ya uchezaji soka. Seedorf, alikuwa akiicheza Botafogo ya Brazil tangu mwaka 2012.

"Ni ngumu kufanya maamuzi ya aina hii, lakini nimeridhishwa na kile nilichofanikisha katika uchezaji wangu. Hapa Botafogo nimefurahishwa sana kwasababu ninaiacha timu ambayo imefuzu kwa ajili ya michuano ya [Copa] Libertadores.

"Nina iacha klabu ambayo kuna fikra nzuri na ari ya hali ya juu.

"Na Ndio nitakuwa kocha pale Milan."
Source : SM

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire