vendredi 20 septembre 2013

Timu ya Taifa ya Burundi itawakosa wengi South africa...



Issa Vidic
Burundi kwenye mashindano ya CHAN 2014 nchi South africa itawakosa wachezaji wengi ambao walikuwa ni viungo kweli kweli kwenye timu ,wachezaji hao  walitowa mchango mkubwa kwa mafahanikio ya timu ya taifa hadi kujinyakuliya tiketi yakucheza kwa mara yake ya kwanza kombe la CHAN litakalo anza mwakani . Jumla ya Wachezaji 18 walio andika historia kwakuifunga Sudan Mjini Khartoum kupitiya matuta ya penalti ambapo kipa Mrundi Arakaza Mc Arthur alifanya kazi kubwa kwakupanguwa penalti 2 kati ya nne na kuiweka pazuri timu yake ya taifa .
Ntibazonkiza saidi

Wachezaji ambao imshafahamika kuwa hawatajiunga na timu ya taifa :

- Kaze Gilbert na Tambwe Amissi wanacheza Tanzania mu Simba.

- Nahimana Claude na Ciza Hussein alie wahi kujiunga na timu hiyo kwa maandalizi watajiunga na Mukura Victory Sports ya Rwanda

- Shasir Ismail atajielekeza Austria (Autriche) hivi karibuni kwani mambo yake ya usajili yanaelekea kufika ukingoni

- Ndayishimiye Christophe ameshajiunga na A.F.A.D ya Ivory Coast,akiwa timu moja na Kwizera Pierrot

- Issa Vidic ilikuwa ajiunge na timu ya daraja la kwanza nchini Ufaransa ,ila habari ambayo habari tuliyo ipata kwa mchezaji huyo ni kuwa anasubiri kwanza acheze CHAN kisha mambo mengi ni baadae...

Arakaza Mc Arthur


- Manirakiza Haruna Lucio ambae alitowa mchango mkubwa kabla nayeye atarejeya kwenye timu yake ya St Eloi Lupopo akiwa pamoja na Afizi.

-Arakaza Mc Arthur amesema kuwa pako timu nyingi za inje zinamuhitaji ila alifahamisha BB kuwa atakuwa na lakusema CHAN itakapo malizika.

·  * Uhamisho rasmi kwa wengine wachezaji kutokea Burundi kujielekeza nje ya nchi :

- Nzokira Jeff atasalia kwenye timu yake ya ASSAD Djibouti Telecom , jana  saa sita mchana ndipo alisafiri nakuelekea Djibouti akiwa pamoja na Andassango Freddy aliekuwa mshambuliaji wa timu ya Lydia Ludic burundi academic.

- Steve NZIGAMASABO tayari kwakusaini rasmi mkataba wa miaka 2 kwenye timu ya Enougou Rangers baada yakuwa alikuwa alisaini Pres contrat ya miezi 6.

- Papy Faty yeye amesalia kwenye timu yake ya Bidvest nchi south africa.

- Ntibazonkiza Saidi kama tulivyowafahamisheni kwenye habari tulizo zichapa kabla kuwa palikuwepo uwezekano akaihma klabu yake ya Cracovie crako nakurudi Spain alipo acha adisi wakati alikuwepo;ni kuwa mwenyewe alitufahamisha kuwa aliongeza kandarasi nyingine na atasalia pale Poland.

- Yameen Selemani bado azidi kungaa’ara kwenye klabu ya El Mereikh ya Sudan japo siku za nyuma kama miezi 5 ya nyuma alikuwa na matatizo yakupewa marupurupu yake (kulipwa) ,ila kwasasa anaendela vizuri.

* Vital’o fc itawapoteza wachezaji wengi mno msimo huu :
Photo : SSC
Demunga na Tambwe
· Girikwishaka John

· Girukwishaka Michel

· Christian Mbilizi

· Ndikumana Lule,wote hao 4 wako kwenye mazungumzo ya lala salama na Kiyovu iliompata Coach mpya ambae ni Kanyenkore Gilbert.

· Nkurunziza D’Amour inasemekana anaweza kujiunga na timu ya St Eloi lupopo ya DRC
. Kaze Gilbert na Amissi Tambwe wao tayari wameshajiunga na Simba .


* Inter Star inaweza kuwapoteza :
Shasir Ismail
-Mussa Sova Ally  ameshajiunga na Kiyovu Sports ya Rwanda .

-Shassir Ismail atajielekeza Autriche kwenye daraja la kwanza , karatasi zake ziko tayari.

-Aime Nzohabonayo ambaye mdaa wowote anaweza kujiunga na T P Mazembe ya DRC



* Atletico inaweza kuwapoteza :
Photo : Trainning session 2013-2014
Pierrot na Christophe.
-Ramadhan ,Ciza , Papa Claude watajiunga na Mukura Vs ila bado wako kwenye mazungumzo ya mwisho

-Christophe Ndayishimiye Yupo AFAD /Ivory Coast pamoja na Pierrot.




* Lydia Ludic Burundi Academic
Photo : Type matembe
Type Bolima Matembe
-Type Bolima Matembe ambae kishajiunga na DCMP ya DRC.

-Andassango Freddy ambae atajiunga na ASSAD Djibout Telecom

- Issa Vidic kuna uwezekano aelekeye ufaransa.

Ratiba ya michuano wiki hii :


*  Jumaa-mosi , tarehe 21/09/2013: mchuano wakutafuta tiketi yakujiunga la Ligi kuu kati ya UNITE & VOLONTAIRES ,saa tisa . Mchuano wa awli Volontaires ilifunga bao 2 kwa 0 ila Unite ya Muyinga walicheza wakiwa 9 uwanjani ,ikisemekana kuwa palikuwepo dosari kwa wachezaji waliyowasilishwa uwanjani siku hiyo.

  * Jumaa-pili,tarehe 22/09/2013,saa tisa : Fainali yakuaniya tiketi yakushiriki kombe la Shirikisho barni Afrika kati ya :
LYDIA LUDIC ACADEMIC - ACADEMIE TCHITE


- Ifahamike ya kuwa fainali ya kombe la Super Primus League imepangwa kuchezwa tarehe 29/09/2013 na ndio siku yakugawa zawadi zote za msimo wa 2012-2013.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire