dimanche 25 août 2013

Vital'o Fc haijawapa Hati za uhamisho wakimataifa Demunga na Tambwe ili watambulike rasmi kuwa wamesajiliwa.

Amisi Tambwe akiangalia mchezo wa leo akiwa ndani ya basi la Simba SC Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi


MWENYEKITI wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage ameondoka jana Jumaa-pili  usiku Dar es Salaam kwenda Bujumbura, Burundi kufuatilia Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) za wachezaji wake wawili, beki Kaze Gilbert na mshambuliaji Tambwe Amissi ambazo zinachelewa kuwafikia.

Rage anapambana ili wachezaji hao waweze kucheza mechi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKT Oljoro mjini Arusha Jumatano, baada ya jana kukwama kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya wenyeji, Rhino Rangers . Wachezaji hao waliosajiliwa kutoka mabingwa wapya wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Vital’O ya kwao, leo walikuwapo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi kuishuhudia timu yao ikilazimishwa sare ya 2-2 na Rhino.
Kocha Mkuu wa Simba SC, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ amesema kukosekana kwa wachezaji hao leo kumechangia matokeo ya sare kwa timu yake.

Kibadeni, ambaye pia alisema kipa Mganda Abbel Dhaira amewaangusha leo kwa kufungwa mabao rahisi, alisema aliwaandaa wachezaji hao kwa ajili ya kucheza jana , hivyo kuwakosa imemvurugia mipango yake.
“Nilitegemea sana kuwatumia wale mabwana leo, lakini kwa bahati mbaya, ITC zao zimechelewa kufika na tumeshindwa kuwatumia, kwa kweli imeniangusha sana,”alisema.
Simba SC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya jana .
Mabao yote ya Simba SC yalifungwa na kiungo Jonas Mkude dakika za 10 na 38 kwa penalti, wakati ya Rhino yalifungwa na Iman Noel dakika 36 na Saad Kipanga dakika ya 64.
Simba SC imeondoka mjini Tabora leo  asubuhi kwenda Arusha tayari kwa mchezo wa Jumatano na Oljoro, ambayo leo imeanza Ligi Kuu kwa kufungwa 2-0 nyumbani na Coastal Union . Ifahamike ya kuwa wachezaji hao walichelewa hata kujiunga na timu hio Mjini Dar kutokana na viongozi wa Vital'o kuchelewa kuwapa passport zao . Duru nilizozipata ni kuwa timu ya Vital'o inadai pesa nyingi sana kwa wachezaji hao wawili kitu ambacho kilicho wastaabisha wachezaji hao nakuomba kuwa kamba iregezwe ili watafte maisha yao . Pengine ujio huo utaza matunda,wait and see...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire