|
The Mafia Entertainment wakiwa mbele ya waandishi habari. |
Msanii Super star kutokea Bongo,mmoja kati ya wakali wa
Omar Nyembo. maarufu kama
OMMY DIMPOZ ilikuwa imepangwa atuwe leo hii mida ya saa tatu asubuhi Jijini Bujumbura kwa Tamasha babu kubwa ilio andaliwa kwa niaba yake na ushirikiano tosha na Wanamuziki wa hapa nchini. Kwa muujibu wa habari tulizozipata kwa wanao anda ujio wake
* The Mafia Entertainment* wamefanya mkutano na waandishi habari asubuhi hii nakuweka wazi kuwa :" Kutokana na moto kuuteketeza uwanja wakimataifa wa ndege wa Kenya , imempelekea
OMMY ambae alikuwa tayari Nairobi kwakusubiri ndege itakayomleta hadi Bujumbura kutowasili tena kwa muda ambao alikuwa alipangilia kuwasili Bujumbura . The Mafia Entertainment inayosimamiwa na
ANZO MAFIA wametubainishia kuwa ifikapo saa tisa ya usiku atakuwa ametuwa kwenye uwanja wa ndege kwani tayari ameshaifanya connection nyingine ya Ugandair ili kuheshimisha muda wa Tamasha inakayo subiri na halaiki ya watu Jijini Bujumbura na sehemu mbali mbali kama UVIRA / DRC na kungineko. " Aliendelea anatufahamisha
Dj Raphan ( Msimamizi wakupasha habari kupitia kampuni hio) kuwa :" Nimeongea na
DIMPOZ akiwa Mjini Nairobi akanibainishia kuwa yupo sawa,na usiku wa leo akimaanisha saa 9 usiku atakuwa tayari Bujumbura kwa show ,na mdaa huo amejielekeza kupumzika kwa JAGUAR ambae nae pia asubiriwa mwa hizi siku 2 kwenye tamasha ya Buja Summer Fest ilio andaliwa na
KIDUM. Amenifahamisha kuwa kadri hali itakavyokuwa anahitaji kusali sala tukufu ya laidi Mjini Bujumbura kwa mara yake ya kwanza " . Ifahamike ya kuwa wanaomchezeaga anakapokuwa kwenye jukwaa (Dancers) wapo tayari Bujumbura . Tamasha imepangwa kwenye ukumbi wa NEW LA GUINGUETE,zamani pakijulikana kama BETHEL CENTER .
* Baadhi ya picha tulizo zichukuwa :
|
Sehemu aliokuwa ameandaliwa kufanya mkutano na Waandishi habari. |
|
Gari aina ya PRADO ndio aliokuwa amepangiwa kupokelewa. |
|
Dancers wa Dimpoz wako tayari Mjini Bujumbura. |
|
Askari polisi watakao linda usalama wa Dimpoz. |
|
Anzo Mafia. |
|
Baadhi ya watangazaji walio hudhuria...
|
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire