Mugani Desire a.k.a General Fizzo , Burundiano... |
MUGANI DESIRE a.k.a Burundiano , Big Fizzo...Mmoja kati ya wakali wa muziki wa Burundi anae ishi Jijini LILLE nchini Ufaransa asubiriwa kwa hamu nchini ifikapo siku ya Jumaa-tano usiku na ndege aina ya Bruxelles Airlines . Kwa mujibu wa habari tulizozipata kwa upande wa viongozi wa Primusic 2013 , walitufahamisha kuwa Msanii huo alipokuwa ziarani Burundi walijaliwa kusaini nae mkataba mungine mwaka huu wa tamasha takribani 4 atakazo ziendesha chini ya uongozi wa Primusic kinyume na zile atakazo ziendesha yeye binafsi kwenye mikataba atakayo ifanya baada ya tarehe 18 /August , tarehe ya fainali ya Primusic 2013 . Ikumbukwe ya kuwa msanii huo mwenye hazi ya ujuzi wakuimba , kuandika nakucheza akiwa kwenye jukwaa amejijengea sifa tele mwaka jana kwenye jumla ya tamasha alizoziendesha kwenye sehemu mbali mbali,alipotoka Burundi nyuma ya mgongo aliacha pini kama : Daima feat Samantha Ndakumisinze, huzuye,Uko wapi , Nakulove ,na ya mwisho kabisa alio acha kwa washabiki wake ikiwa ni * Mama * . Karibu sana nyumbani...
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire