mardi 22 janvier 2013

Kinshasa : -Abdul Razak fiston:" Mambo yangu shwari pande za Congo Brazza."

Fiston Abdul razak ....





Jana usiku tulifanya mahojiano na Mchezaji wa Burundi ambae alichukuwa mwaka jana tunzo mbili (Mfungaji na Mchezaji bora mwaka 2012). Fiston Abdul Razak alitufahamisha mengi kuhusu maendeleo yake akiwa nchini Congo-brazzaville.Tulianza kumsalimia,akatujibu :
  • Fiston Abdulrazaq

    powa kaka labda nyinyi huko.
    • Amidou Hassan

      tupo sawa,nambie uko pande zipi kwa mda huu?
      • Fiston Abdulrazaq

        hivi nipo kinshasa tulikuja kucheza ma match amical tumeshacheza match tatu bado mbili kisha turudi brazza ville kisha tutaenda tena gabon hizozote ni macth a mical tunajiandaa kwenda ghana mwezi wapili cpslg
        • Amidou Hassan

          cpslg maana yake nini? na tayari umesajiliwa ao bado wanakupima? timu inaitwaje?
          • Fiston Abdulrazaq

            maanayake (champions league) tayari nimesajiriwa nakatika hizo match tatu nimeshafunga 2 but. Timu inaitwa (Diable Noirs) ya Brazza ville.
            • Amidou Hassan

              mlicheza na timu gani nataka niandike vitu vya uhakika kwa ajili uku habari za mitaani ni nyingi tena uongo mtupu.


              • Tumecheza match ya kwanza na As dragon tumeifunga 1-0 mimi ndo nimefunga match ya pili tumecheza na v.club tumepoteza 2-1 ila kwa kuibwa saana nakupewa goal yauwongo baada yakumnyanganya kipa mpira mikononi hadi kaumia.match yatatu tumecheza leo hii na (mk) sijuwi maanayake kwaurefu waiita hivohivo(eme ka)tumeifunga 1-0 mimi ndo nimeifunga.na kesho tutacheza na selection ya junior ila sizani kama hiyo ntacheza sababu ya mchoko wa match tatu mfululizo tena ngumungumu yani mwili unauma sana.




                N.B :Tulipenda kusahihisha habari hii gisi tulivyo ipata kutokana na baadhi ya Watangazaji ambao wamevuma ao wanahitaji kuvuma kwakuziandika habari bila kuwa na uhakika na habari wanazo ziandika bila kuwa na ushahidi tosha.Burundi beat Ent inawa ahidi kuwapeni habari zisizokuwa na mchangana zenye manufaa ya aina yake.Habari ndio hio...

                  1 commentaire: