mercredi 7 août 2013

Breaking news :Moto wateketeza uwanja wa ndege Kenya

Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ukiteketea

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta umefungwa baada ya moto mkubwa kutokea katika uwanja huo mjini Nairobi. Kwa sasa moto huo umeweza kudhibitiwa.

Rais Uhuru Kenyatta amewasili katika uwanja huo na anatarajiwa kuhutubia waandishi wa habari baadaye. Hadi kufikia sasa hakuna ripoti zozote za majeruhi . Mwandishi wa BBC katika uwanja huo amesema kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka katika eneo la kuondokea na kuingilia wageni.

Mamlaka ya uwanja huo imesema kuwa tayari watu waliokuwa katika eneo hilo wameondolewa.

Imesema kuwa baadhi ya operesheni za uwanja huo zimekatizwa huku ndege zinazoingia katika uwanja huo zikielekezwa kutua katika viwanja vingine ndege kama vile Entebe, Dar es Salam ,Kigali, Mombasa na kwingineko nchini Kenya.

Baadhi ya safari za ndege kutoka uwanja huo pia zimeahirishwa.

Mwishoni mwa wiki jana baadhi ya wenye maduka ya Duty Free katika uwanja huo walifurushwa baada ya serikali kusema kuwa leseni za wenye maduka zilikuwa zimepitwa na muda.

Hata hivyo chanzo cha moto bado hakijabainika.
Source : BBC

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire