jeudi 4 juillet 2013

VITAL'O FC kwenye ndege 1 na Timu ya taifa ya Sudan zasubiriwa Bujumbura kesho Ijumaa (Vendredi).

Photo : VITAL'O are cecafa 2013 club champs..last night in Sudan
Usiku wa Jumaa-tatu ,shangwe na furaha kubwa kwa timu nzima baada yakukabidhiwa kombe.
Baada yakutwa kombe la kwanza kwenye mashindano ya CECAFA KAGAME CUP,na kuingia tayari kwenye heshma nakujiorodhesha tayari kwenye historia ya mpira nchini Burundi na kwenye kanda ya afrika mashiriki na kati . Vital'o Fc na jopo nzima walioshirikiana kwenye msafara huko kusini mwa Sudan wako kwa mdaa huu Mjini Karthoum toka siku ya Jumaa-ine,kutokana na ukosefu wa ndege yakuwarudisha mapema kabla tu ya fainali walio icheza Jumaa-tatu nakuilazimisha APR FC ya Rwanda kwa bao 2-0 kwenye fainali .
Walipo wasili jana kwenye uwanja wa ndege wa Karthoum/Sudan.

Vijana hao wa KANYENKORE KAGABO GILBERT alias YAOUNDÉ wanasubiririwa mchana wa siku ya Ijumaa kwenye uwanja wakimataifa wa ndege wa Bujumbura wakiwa kwenye ndege moja na wachezaji wa timu ya Taifa ya Sudan itakatomenyana na Burundi siku ya Jumaa-pili 7/July/2013 kwenye Uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore duru ya mtowano na yamwisho kwa upande wa michuano ya wachezaji wanaocheza soka la nyumbani maarufu kama CHAN.
Asubuhi wakiwa wanapata chai (KHARTHOUM)

Endapo Burundi itashinda tukujumuisha michezo hio muhimu miwili basi moja kwa moja itakuwa imejiandikia ingine historia yakucheza michuano ya africa ya wachezaji wanaosakata gozi la nyumbani (CHAN). Hofu na dukuduku kwa upande wa wadau wa soka kwa wachezaji wa Vital'o Fc ambao wako kwenye timu ya Vital'o Fc kutojinowa na wengine ipo na inadhihirika kwani watafika Ijumaa na mchuano umepangwa Jumaa-pili.
Kombe ndio hilo

Habari kutoka Karthoum imebainisha kuwa Mkufunzi mkuu wa Vital'o Fc Yaoundé anaendelea anawapa mazoezi baada ya kuwa bado wana michuano ya Ligi kuu inayowasubiri nchini , kwa muujibu wa THEODORE NTUNGA,mtangazaji alioko kwenye msafara huo ( R t n b ),alitufahamisha kuwa :" Vital'o Fc walipumzika siku ya Jumaa-ine (mardi) ,ila jana na leo kwenye mpango wa Coach imepangwa wafanye mazoezi katika hali yakujiweka sawa ili watakapo rudi nchini wawe kwenye hali nzuri yakukabiliana na Primus League."

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire