dimanche 1 septembre 2013

Nigeria : Unamkumbuka Jay Jay Okocha Kutoka Nigeria, Mkali Huyu Wa Soka Sasa Ameamua Kubadilisha Fani,amejiingiza katika tasnia ya filamu kama mtayarishaji,



Majek Fashek, Jay Jay Okocha
Augustine Jay Jay Okocha, Mwanasoka kutoka Nigera ambaye amejipatia umaarufu mkubwa duniani kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kucheza soka kitaifa na kimataifa, aameamua kubadilisha fani baada ya kuwa katika soka kwa miaka mingi sasa.

Staa huyu wa mpira, amejiingiza katika tasnia ya filamu kama mtayarishaji, na sasa yupo katika mchongo wa kutayarisha filamu kuhusu nyota wa muziki wa reggae anayefahamika kwa jina Majek Fashek ambayo imeandikwa na Charles Novia iliyopo katika hatua za awali za utayarishaji wake.

Baadhi ya vipande vya filamu hii vitafanyika huko New York Marekani mwezi wa kumi, ambapo wahusika katika nafasi za filamu hii ni Francis Duru, Sam Dede, Stella Damascus pamoja na waigizaji wengine wakali kutoka Nollywood.


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire