lundi 8 avril 2013

Dar Es Salaam: STEVEN KANUMBA atimiza mwaka toka alipofariki...


Jana tarehe 7/April/2013  ni mwaka ulitimia tangu msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Charles Kanumba kuiaga dunia. Marehemu Kanumba alifariki dunia alfajiri ya Jumamosi Aprili 7, 2012 akiwa na umri wa miaka 28, baada ya kile kilichodaiwa kuwa ni ugomvi wa kimapenzi na rafiki yake wa kike, Elizabeth Michael kwa jina maarufu “Lulu” na kuzikwa Aprili 10, 2012 na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na wengineo.
Mpaka sasa bado hajatokea msanii wa kuziba pengo aliloliacha marehemu katika tasnia ya filamu.

Ujumbe uliopo katika kaburi la Kanumba.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire