dimanche 1 décembre 2013

BOTCHUM , Producer wa IKOH MULTISERVICE aliwasili jana tarehe 30/11/2013 Bujumbura akitokeya DUBAI...

Botchum pichani na familia yake...
Baada yakuifanya ziara ya siku kadhaa akiwa Dubai Kwizera Freddy Khalhed maarufu BOTCHUM jana usiku mida ya saa mbili usiku ndipo aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bujumbura . Producer huyo mwenye hadhi ya kimataifa kulingana na kazi nzuri anayo ifanya mdaa mrefu alipokelewa jana na jopo la Watangazaji na familiya yake bila kusahau CREW ya IKOH MULTISERVICE . Alipofika uwanja wa ndege akiwa ameonekana na uchovu wa safari hakusita kudhihirisha furaha na kujivuna kuona amerudi nchini mwake na zawadi tosha ya mafaanikio kwa jamii ya Burundi hususani wa Producer wengine waliyobaki nchini .
Pichani : Dj Raphan , AH & Aisha Amuri...

Alitwambiya :" Namshkuru Mungu kuona nimefika salama , na ninawashkuru kuona mlifkiriya kuja kunipokeya , nibahatikiwa kuyafwatiliya mafunzo ya kazi ninayo ifanya hapana shaka kuwa itakuwa njiya mbadala kwa ufanisi wasisi wote kwakuikuza tasnia ya muziki nchini , ninapangiliya kuanda kikao na wenzangu ili tutasmini kwa pamoja kipi chakufanya ili tuchangiye pamoja mafunzo niliyo yapata , Burundi tunaweza ili inatubidi tusome zaidi kwani technolojia kila siku inasonga mbele ". Hiyo ni gari ya IKOH iliyokuwa tayari toka saa kumi kumsubiriya BOTCHUM uwanja wa ndege .

Aliongeza kusema :" Shukran za dhati kwa Mr IKOH kwa  jitiada zake zote zakuyaleta mabadiliko nchini ." Alimaliziya :" Tulipokuwa jana siko tulipo leo, leo tulioko tukishikama kwa pamoja  hapana shaka kuwa kesho patakuwa pazuri zaidi."
 

Huu ni mfano mungine wa malengo ya Kampuni ya IKOH MULTISERVICE kuleta mabadiliko nchini ,baada yakutangaza rasmi kuanza kwa Kampuni ya '' You'll Love Changes '' kuziba pengu na kulinda heshma ya wasanii wa bongo movies kukwamishwa nakuingiliya kati kugharamiya kila kitu kilichohusikana na ziara yao hasa hasa kuhusikana na kuwalipiya Hotel namengineyo , Mr H anasema hatoishiya hapo kwani yeye malengo yakuanzisha Kampuni ya IKOH ni kuleta mabadiliko nchini...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire