dimanche 7 juillet 2013

CHAN 2014: Burundi 1-1 Sudan.

Pichani : Rashid Leon akitaka kupiga krosi kuelekea lango la Sudan...
Mchuano wa duru ya awali ya Wachezaji wanao sakata gozi la nyumbani maarufu kama CHAN ulichezwa leo kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore ambapo Burundi ilikuwa imeipokea nchi ya Sudan . Ifahamike ya kuwa ni mchuano wa mwisho timu moja kati ya hizo mbili itafudhu moja kwa moja kuchuana kombe la CHAN 2014 nchini Africa ya Kusini. Mtanange wa leo ulishughudiwa na wapenzi wasiokuwa wadogo tukilinganisha pande zote za uwanja waliokuwa waliwasili kushughudia mchezo huo ambao ulikuwa ni muhimu sana kwa nchi yetu japo bado tunasubiri mchuano wa marudio. Intamba Murugamba ilipata nafasi ya kwanza yakupachika bao kipindi cha kwanza ila bahati mbaya mshambuliaji TAMBWE AMISSI akuitumia vyema nafasi hiyo nakujikuta ameugonga mpira goalkeeper wa Mamba za Nil kifuani. Mnamo dakika ya 20 ndipo Tambwe Amissi huyo huyo aliandikisha bao baada kidogo safu ya nyuma kuzembea kwa upande wa Sudan. Dakika 7 baadae yaani dakika ya 27 ndipo Issa Vidic alizuba kidogo nakumuangusha mshambuliaji wa Sudan na Referee kutoka Rwanda hakusita nakuwazawadia papo hapo penalti iliokuja kufungwa na NADIR ELTAYEB ,kipa wa Burundi ARAKAZA Mc Arthur hakuona wapi mpira uliopita . Kipindi cha pili hapakuwa mabadiliko yoyote kwa upande wa ubao ila kilicho onekana nikuwa kuzoweyabna mtindo wakucheza kuliko kudogo kwani kati ya wachezaji 18 waliokuwa kwenye orodha leo , wa 5 ni wapya na ikawaweya ngumu sana kuweza kuonyesha mpira mzuri sana kama tulivyokuwa tunasubiria.
Shassir,kiungo wa Inter Star...

Kwa muujibu wa naibu Coach wa AMARS NIYONGABO alibaini kuwa :" Kwa kweli tulijitaidi kadri tuwezavyo ila bahati hatukuwa nayo,tulikuwa na upungufu wawachezaji 5 ambao walipata nafasi nyeti yakusaini mikataba na timu za nje nikizungumzia kama (Fiston Abdul Razzak-Rayon sport ya Rwanda,Manirakiza Lucio-Lupopo DRC, Steve Nzigamasabo-Enugu Rangers Nigeria,Emery Kadogo ambae hachezi kwasasa mkataba wake kwenye timu ya Diables Noirs ya Brazza ville ni kama umesimama...). Hawakutushinda sana,tumeona wanavyocheza,duru ya marudiano tutajituma tuone nini chakuongeza ,nini chakupunguza ili twende kule tukiwa na stamina yakutosha. Matokeo ya 1-1 sio mazuri sana kwani wao wamekwenda na ushindi ila tutakaa chini na tutasmini mbinu ipi tutakayo itumia ili tujiweke sawa na mpambano wa marudiano,nazitowa shime kwa wachezaji wote ,Shassir ndio mchuano wake wa kwanza ila alionyesha kiwango chakuridhisha mno." Mchuano wa marudiano ni mnamo wiki 2 akipenda Mungu Mjini Kharthoum...

11 walio anza uwanjani kwa upande wa Intamba Murugamba:

 (1)ARAKAZA Mc Arthur . (3) Rashid Léon , (17) Hakizimana Hassan L'Homme(C),(15)  Kaze Gilbert , (14) Issa Hakizimana , (6) Nduwarugira Christophe, (10) Shassir , (2)Duhayindavyi Gael , (13) Ndarusanze Claude , (11) Aime Nzohabonayo , (9) Tambwe Amissi.

Walio kuwa nje :

(18)Rugumandiye Yvan , (8) Nkurikiye Leopold Kaya , (5) Nsabiyumva Frederick , (16) Ndayishimiye  Christophe ,(7)  Nahimana Claude , (12) Ndayiragije Abdul Razzak.


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire