Ozil |
KIUNGO Mesut Ozil amewasili katika klabu yake mpya jana, Arsenal tayari kuanza kumtumikia Arsene Wenger anayekabiliwa na tatizo la wachezaji wengi majeruhi.
Mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 42 ataanza mazoezi leo makao makuu ya klabu, Colney London kwa mara ya kwanza tangu ahamie akitokea Real Madrid. Na Wenger anajiandaa kumtumia mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani katika mchezo dhidi ya Sunderland Jumamosi baada ya Tomas Rosicky kurejea kwenye mechi ya timu yake ya taifa akiwa majeruhi .Mwendeshaji hodari: Ozil alidhihirisha tena uwezo wake alipoiongoza Ujerumani kuilaza 3-0 Faroe Islands .
Mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 42 ataanza mazoezi leo makao makuu ya klabu, Colney London kwa mara ya kwanza tangu ahamie akitokea Real Madrid. Na Wenger anajiandaa kumtumia mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani katika mchezo dhidi ya Sunderland Jumamosi baada ya Tomas Rosicky kurejea kwenye mechi ya timu yake ya taifa akiwa majeruhi .Mwendeshaji hodari: Ozil alidhihirisha tena uwezo wake alipoiongoza Ujerumani kuilaza 3-0 Faroe Islands .
Akiwa kwenye kikosi cha Germany |
Rosicky anaungana na Thomas Vermaelen, Mikel Arteta, Alex Oxlade-Chamberlain, Lukas Podolski, Abou Diaby na Yaya Sanogo katika chumba cha majeruhi wa klabu hiyo. Habari njema kwa Wenger ni kwamba, Theo Walcott na Jack Wilshere wanatarajiwa kuwa fiti kwa mchezo wa Jumamosi baada ya kushindwa kuichezea England mjini Kiev.
Chamberlain na Ozil |
Wilshere alitolewa katikati ya kipindi cha pili na Walcott alitolewa baada ya kuumia akipambana na Oleksandr Kucher.
Akiwa na Podolski,Mjerumani mwenzie... |
Lakini wote wanatarajiwa kucheza dhidi ya timu ya Paolo Di Canio mwishoni mwa wiki hii.
Habari zinazo zungumzawa kwenye timu hiyo ni pamoja na :
UHABA wa washambuliaji umeongezeka kwa Arsene Wenger, baada ya Yaya Sanogo kuumia na kuifanya Arsenal sasa ibaki na mshambuliaji mmoja tu wa kati aliye fiti.
Sanogo - ambaye kwa sasa ni mshambuliaji chaguo la pili Arsenal- amerejea katika klabu hiyo kutoka kuichezea timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21 akiwa majeruhi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 atafanyiwa matibabu makini makao makuu ya klabu, Colney, London kuhakikisha anakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa mwishoni mwa wiki na Sunderland - ambao utakuwa wa kwanza pia kwa mchezaji mpya ghali wa klabu hiyo, Mesut Ozil aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 42 kutoka real Madrid. Presha: Olivier Giroud sasa ndiye mshambulaji pekee wa kati aliye fiti katika klabu hiyo . Majeruhi hayo yanamaanisha, Olivier Giroud anabaki kuwa mshambuliaji pekee wa kati aliye fiti katika klabu hiyo kuelekea mchezo wa Jumamosi Uwanja wa Light.
Sanogo, aliyesajiliwa kutoka Auxerre majira haya ya joto, alisajiliwa na Wenger kwa ajili ya kuandaliwa aje kuisaidia klabu baadaye, lakini uhaba wa washambuliaji umefanya apewe majukumu mapema kikosi cha kwanza . Klabu hiyo ilikwama kuwasajili Luis Suarez, Gonzalo Higuain, Wayne Rooney, Karim Benzema na Demba Ba hivyo kumuachia wakati mgumu Wenger.
Lukas Podolski anaweza kucheza badala ya Giroud, lakini naye anatakiwa kuwa nje kwa miezi mitatu sababu ya maumivu ya nyama, wakati Nicklas Bendtner - ambaye klabu ilijaribu kumuuza wakati wa dirisha la usajili, hayuko fiti kwa mechi. Mesut Ozil ndiye mchezaji pekee mkubwa aliyesajiliwa na Arsenal msimu huu . Mbali ya Sanogo, Wenger anaweza kuwatumia Theo Walcott katikati, wakati kidna wa miaka 17, Chuba Akpom anaweza kuanzia benchi.
Habari njema kwa Wenger ni kurejea kwa Thomas Vermaelen kuanza mazoezi kamili. Nahodha huyo wa klabu, amekuwa nje mwanzoni mwa msimu kwa sababu ya maumivu, lakini alianza mazoezi mepesi mwishoni mwa mwezi uliopita.
Lakini Vermaelen ameanza mazoezi kamili na bila shaka anarejea kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Wenger. Ameanza mazoezi kamili: Thomas Vermaelen anatarajiwa kuongeza nguvu Arsenal .
Hakuna namna : Lukas Podolski (kushoto) ni majeruhi wakati Bendtener ( kulia ) haamini tena...
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire