vendredi 19 avril 2013

QUESTION G, WAFANYAKAZI KWA VITENDO NA SIO KWA MANENO.



Mwishoni mwa juma lililopita kundi la Question G, lenye Maskani yake tarafani Bwiza katika manispaa ya jiji la Bujumbura, wame rikodi video zao mbili kwa pamoja na kudaikuwa hawafanyi kazi kwa maneno bali kwa vitendo.

akichonga mawili matatu na Ikoh.biz, Josdy Prince mmoja miongoni mwa vijana wanaunda kundi hilo amesema waliahidi kuwa mwaka huu watafanya kazi kwa vitendo, na ndicho wanachokifanya kwa sasa, baada ya kurikodi

Audio ya wimbo wao 'Inauma sana' na kumshirikisha msanii wa Burundi anaekichanga huko Afrika Kusini mshiriki wa tuzo za Kora Awards 2012, Chris Dizzo, na sasa wapo jikoni kuipika video hiyo ambayo hata hivyo itakuwa tayari siku za usoni. Wimbo mwingine unaotengenezewa video kwa sasa ni wimbo wa Bella na Shella, wimbo wa kundi hilo.


Question G ni moja miongoni mwa makundi yaliowahi kutikisa jiji la Bujumbura katika miaka iliopita baada ya kujizolea mashabiki wengi kutoka katika tarafa mbalimbali za manispaa ya jiji la Bujumbura.


Vijana wa kundi hili wamekuwa wakipata mialiko ya huku na kule kwa ajili ya kuendesha burudani ambapo hivi karibuni walikuwa Mkoani Gitega kukonga myoyo ya wapenzi wa Muziki katika eneo hilo la nchi.


Source: Ikoh

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire