samedi 20 avril 2013

Jarida la Times kumpa Balotelli heshima ya kipekee ya kumjumuisha kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa na mvuto duniani...


Taswira ya mshambuliaji wa kimataifa wa Italia anaechezea klabu ya Ac Milan Mario Balotelli kwa muda mrefu imekuwa ikihusishwa na utukutu ambapo vyombo vya habari vimekuwa vikichora picha mbaya za huyu jamaa kutokana na vituko vyake anavyovifanya kila kukicha.

Hayo yote hayakulinyima Jarida la Times kumpa Balotelli heshima ya kipekee ya kumjumuisha kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa na mvuto duniani, ambapo kwenye orodha hiyo amekua mwanasoka pekee na mmoja kati ya wanamichezo watatu pekee waliojumuishwa kwenye orodha hiyo akiwemo mchezaji kikapu Lebron James na mcheza tenis toka China Li Na.


Balotelli amepewa heshima hii baada ya kuwa mmoja wa wanasoka maarufu wanaotajwa sana kwenye vyombo vya habari kwa sababu mbalimbali lakini kubwa likiwa vituko vyake , vituko hivi vya Balotelli vimemfanya kuwa na taswira yenye nguvu na inayotambulika ulimwenguni kote jambo ambalo limemuongezea umaarufu.




N.B : Orodha hii ni kwa mujibu wa TIME, na kwa maelezo zaidi tembelea  http://time100.time.com/2013/04/18/time-100/slide/all/

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire