Baada ya hali yautata inayokabili uongozi wa Shirikisho la mpira nchini Burundi (FFB) na baadhi ya viongozi wa klabu mbali mbali kwenye shirikisho hilo kuhusikana nakutochezwa kwa baadhi ya michuano ya ligi A na B iliokuwa imepangwa kuchezwa wiki mbili zilizopita na mzozo huo kuingiliwa kati na Wizara ya Vijana Michezo na utamaduni kusitisha michuano hio hadi kutowa amri yakuvifunga viwanja vyote na kuomba pafanyike uchunguzi wa kina ili swala nzima lipatiwe ufumbuzi ni kuwa kwa sasa barua tayari imetoka yakuruhusu kuchezwa kwa Ligi A na B nchini michuano ya ligi ya kwanza na ya pili kuendelea ikiwa imeingia kwenye duru ya marudiano . Mzozo uliokuwa ilikuwa kutochezwa michuano ambayo kiongozi wa FFB mama Lydia NSEKERA alikuwa ameamuwa ichezwa kinyume na Kombe la Raisi lililo kuwa limepangwa kuchezwa kama tulivyo wafahamisheni siku za nyuma . Ivo basi baadhi ya viongozi wa klabu tofauti wakawa wameamuwa kufanya mgomo nakuomba serekali kuingilia kati kwani muhula wa mama Lydia NSEKERA tayari ulishafika ukingoni . Suluhu tayari imepatikana kwani hapo jana imetolewa kalenda ya michuano itakayo anza kuchezwa kuanzia kesho . Je! Michuano hio itachezeka? kwani hadi mdaa huu tunaskia bado kuna Viongozi wanagoma timu zao kucheza hadi pawepo uchaguzi wa kiongozi mpia wa shirikisho lenyewe . Ikumbukwe ya kuwa tarehe ya uchaguzi imepangwa tarehe 5/may/2013 . mchuano wa marudiano kati ya Lydia Ludic Burundi Academie na DC Motema pembe umepangwa kuchezwa siku ya Jumaa-pili insha'allah...
Ratiba ya michuano ,wiki ya 13 na 14 (Phase retour) :
* Alkhamis (Jeudi) , tarehe 11/April :
Saa nane : LLB Academic - Academie TCHITE
Saa kumi : Inter star - Espoir Mutimbuzi
* Jumaa-mosi (Samedi) : tarehe 13/April :
Saa tisa : Messager Ngozi - Muzinga
Saa tisa : Flambeau de l'Est - Atletico Olympic
Saa tisa : Royal - Flamengo fc
* Jumaa-tano (Mercredi) :
Saa nane : Prince Louis - Atletico Olympic
Saa kumi : Vital'o fc - Royal fc
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire