mardi 19 mars 2013

Durban : -KENNY BLUE : "Kwenye msafara wa mamba na kenge zimo"


                                                                                      
SINDAYIGAYA ABDUL RAZAK a.k.a Kenny Blue ambae anazoweleka sana kwa kuondoka na mitindo yakisasa auliziwa Jijini Durban nchini Africa ya kusini (south africa) . Kenny Blue kabla yakutoka Burundi alikuwa tayari na nyimbo tofauti tofauti ambazo hadi mdaa huu zinatamba kwenye anga ya burundi flava, pini hizo ni pamoja na 'Kosa langu ft Dj pro kwa Big base (Menya media records) , Nenda ft Chanella , Rasta man ft Yoya , Promiss ft Kebby (M.A production) Alitufahamisha kuwa yuko anafanya kazi na anasoma muziki pande zile , mwezi uliopita aliachia audio ya pini inayojulikana kwa jina la 'TINGISHA' feat M.Lee ni Msanii kutoka Nigeria, yuko anakimbizana kuitengenezea picha (video) yake ili awaonyeshe washabiki wake kuwa bado yupo kwenye msafara wawaimbaji wa Burundi ambao wanaendelesha kazi zao za mziki wakiwa nje ya nchi. Alitufahamisha kuwa :"Kwenye msafara wa mamba na kenge zimo,na maanisha kuwa japo hatujaaminika sana ki muziki,siku iko,nina imani nitakapo teremka Burundi ntawaonyesha ujuzi gani nilio utowa pande hizi kwani uku ni kazi kwenda mbele usiku na mchana. Baada ya clip kutoka naitaji kuachia nyingine nyimbo mpia , bado ingali kwenye karatasi..."

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire