Royal fc wakiwa Kiganda / Muramvya |
Bujumbura : Prince louis 0 - 1 Flambeau de l'Est
Muramvya : Royal Fc 0 -1 Vital'o fc
Ifahamike ya kwamba pambano hizo mbili zilichezwa uku zingine timu hazikupambana kutokana na baadhi yazo kuwa zimeshamaliza idadi ya pambano 11 za duru ya awali (Aller) . Vital'o yao ilikuwa ni match ya mwisho,Royal fc inasalia na match itakayocheza na Flamengo ifikapo siku ya Jumaa-pili saa kumi jioni . Prince Louis itapambana na Atletico olympic siku ya Jumaa-mosi saa kumi match yao ya mwisho . Huo utakuwa ni mwisho wa Duru ya awali,akipenda Mungu tutawashushia msimamo kamili ifikapo Juma-pili usiku baada ya pambano lakuifunga duru ya awali . Kumbuka ya kuwa katika ya wiki mkoani Ngozi Messager ya Ngozi ilikwenda sare na Espoir ya gatumba 1-1 . Jumaa-tano Inter Star ilifungwa 2-1 na Academie Tchite . Siku hio hio Kiongozi wa Aigles Noirs ya Makamba aliendesha mkutano na waandishi habari nia na madhumuni ya mkutano huo ilikuwa nikumjibu Mwanamama Lydia NSEKERA baada ya mkutano alio ufanya mwanzo nakuzipeleka shutma kuwa kuna Viongozi wa ngazi za juu (Serekalini) wanataka kuchanga siasa na michezo (soccer) hivo basi ilikuwa ni fursa kwake kuwakumbusha viongozi wa Timu mbali mbali kuwa wakati umewadia wakukata uongozi wa Lydia NSEKERA kwani mdaa wake wakuongoza umefikia ukingoni,sasa inabidi pafanyike uchaguzi ili mpira uchukuwe picha nyingine kwani kuna mambo mengi yanayopu uziwa na japo twafahamu kuwa mpira ni chombo mojawapo kinachokutanisha watu na kinacho leta amani nchini,alisema NDIKURIYO REVERIEN aliendesha mkutano huo (Point de press) kwenye Source du Nil Hotel . Leo tarehe 9/March/2013 saa kumi Atletico Olympic itamenyana na Prince Louis . Kinyume na match hizo za mwisho zitakazo fwata ni match za kombe la Raisi zilizopangwa kuchezwa kuanzia tarehe 30/March/2013 . Wabalozi wetu Vital'o fc na Lydia Ludic Burundi Academic watapambana match zao za awali kati ya tarehe 15,16,17/March . Vital'o fc itaanzia Burundi kwa kuipokea Enougou Rangers kutokea Nigeria ,uku LLB itapepetena na D.C Motema Pembe kutokea DRC ,ila kuna habari zinasema kuwa endapo Waziri wa Michezo wa jamuhuri ya Demokrasia ya Congo hatoeshimu amri ya Viongozi wa FIFA inayo omba kuacha kila timu inayoshiriki kwenye michuano ya Africa kuchezea kwenye viwanja vyao binafsi baada ya siku 5,Timu zote za Congo zitafutwa na inaweza kuwa ni afueni kwa LLB kujishindia kwa ushindi wa Chee (Forfait) . Waziri huo yeye apendekeza match zote zichezwe kwenye uwanja wa taifa jijini Kinshasa ,na huku Viongozi wa Timu shirika zinapinga hatua hio na zikawa zimepeleka malalamiko yake kwenye Shirikisho la Dimba Ulimwenguni FIFA .Tusubiri... LLB toka alkhamis wameingia kambini,kuna habari zinasema kuwa watapeleka Wachezaji 14 Jijini Kinshasa,sasa tunajiuliza kwanini wapeleke Viongozi wengi na japo wao hawaendi kucheza ? Kumbuka kuwa Jijini Kigali walipeleka Wachezaji 17 . Sasa kwanini kama ni kweli wapeleke wachezaji nusu na japo wako na wakuenea? Wait and see...
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire