jeudi 1 août 2013

Kaze Gilbert Demunga amejielekeza leo Dar Es Salaam kuongea na viongozi wa Simba SC.

Kaze Gilbert Demunga
Beki wakimataifa kutoka Burundi Kaze Gilbert maarufu  Demunga leo hii amesafiri kwa ndege aina ya kenya Airways kuelekea nchini Tanzania kwa mazungumzo yakusaini mkataba na klabu ya Simba Sports club ya pande zile. Kama tulivyokuchapieni kwenye ukurasa wa habari zihusuzo uhamisho wa wachezaji wa Burundi apo kabla kuwa kijana huo anaweza kujiunga na Simba ya Tanzania,ni kuwa mpangilio mzima waweza kukamilika kwani leo hii ndipo alipojielekeza kwenda kuonana na viongozi wa timu ya Simba ambayo ilikuwa imemsajili Tambwe Amissi mfungaji bora hadi mdaa huu kwenye Primus league na bao 19,na vile vile kuteuliwa kama mfungaji bora kwenye mashindano ya Cecafa kagame Cup yaliomalizika na Vital'o Fc  kutwa ubingwa wa mara yake ya  kwanza.

  Tulipo hojiana na Demunga alituwekea wazi kuwa :" Kwanza nafurahi kuona nilifunga bao langu la kwanza kwenye timu ya taifa,bao ambalo limepelekea nchi yangu kuelekea kwenye mashindano muhimu yakikanda maarufu CHAN , pili Burundi kwasasa imeanza kurudisha heshma kwa upanda wa soka,kuona kuwa tumeanza kukodolewa macho na klabu za inje hii ni hali nzuri yakujivunia,naomba viongozi watoke kwenye ukimya watupe sapoti ili tufike mbali zaidi." Demunga anaweza kuwa mchezaji wa 3 wa Vital'o Fc kusajiliwa official mwaka huu baada ya Nzigamasabo Steve aliejielekeza kwenye klabu ya Enugou Rangers ya Nigeria, Tambwe Amissi ambae hatma yake haijafahamika kuwa aweza kutuwa Simba ao Arabia Saudite.Tunamtakia kila la kheri na fanaka...

Cecafa Kagame Cup/   Dar Es Salaam.
Uchunguzi wa kina kwa upande wa uhamisho bado unaendelea...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire