mardi 29 janvier 2013

Wameamuwa kwanza kuhamisha soko kwenye uwanja wampira wa Cotebu...


Asubuhi ya leo waliokuwa wanafanya kazi sokoni,nazungumzia waliopoteza mali zao sehemu ile walikutana kwenye uwanja wa mpira wa Tempete kwa mualiko wa syndicat ya wafanya biashara (Sygeko)  inaongozwa na Mh  Audace BIZABISHAKA. walianza naumuomba mungu baada ya hapo ndipo walianza kufikisha ujumbe toka kwa tume ilio undwa na makao makuu ya raisi wa 2 wa nchi ya Burundi,alizungumza kuwa :" Kwa muda tumependa kuwafahamisha kuwa soko tunaiyamisha kwenye uwanja wa Cotebu, pembezuni mwa nyumba ya makao makuu ya chama madarakani Cndd,Fdd,kwa muda huu tulipenda tena kuwafahamisha kuwa kuna bidhaa ambazo bado zipo sokoni tunataka tu unde tume ya watu 6 kwa kila tarafa kwa ushirikiano na Askari polisi kuingia sokoni ili kuokowa bidhaa ambazo hazikupatwa na moto,ila itawalazimu wawe na vitambulisho rasmi. Aliwaomba wote waliofika hapo kujiorodhesha na nafasi waliokuwa wanauzia bidhaa zao,vitu walivyokuwa navyo na kopi yakitambulisho chao. kwa ujumla watakuwa watu 24 kwakuongeza 15 ambao watafwatilia kwa kina mpango huo." Walio endesha mkutano huo walikuwa mara kwa mara wanafahamisha wafanya biasha hao kuwa ' Tout ce que nous avions,c'est dieu qui nous avait benis.il fera encore.L'essentiel :restons solidaires et soyons forts." Wakimaanisha :" Tulivyokuwa navyo vyote,atatupa tena.Kikubwa tubaki wamoja na tujikaze sana." Ila lakufahamu ni kuwa wengi kati yawalio hudhuria hapo walilamika kwa sauti ya juu kuwa wanahitaji kusalia kwenye na fasi walizokuwa nazo,kazi bado ingali.Wait and see...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire