Siku ya Ijumaa na Jumaa-mosi tarehe 7 na 8 February 2014 kwenye ukumbi wa Panoramique (Celexon Hotel ) , barabara ya JRR Mjini kati ndipo patafanyika Tamasha mbili za uanzilishi wa Club mpya (Boite de Nuit ) . Ifikapo Ijumaa pameandaliwa Tamasha ya Buja Surprise Friday Party , Jumaa-mosi itakuwa Saturday Night Live ambapo Dj kutoka nchini Kenya anae julikana kwa jina la DJ PIERRA pichani kwenye bango , DJ T.T kutoka Kampala Uganda na DJ Noah kutoka Burundi watakonga nyoyo za Washabiki watakao jumuika kwenye usiku huo . Duru kutoka kwa DAN mmoja kati ya walio anda ujio huo na kuweka mazingira sawa ametufahamisha kuwa :'' Kila kitu kiko sawa , na tunaomba watu wafike kwa wingi kutupa sapoti , tunaimani kuwa mazingira yatakuwa mazuri .''
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire