mercredi 5 février 2014

Matokeo ya Wiki ya 8 Ligi ya taifa nchini Burundi (Vital'o Fc 0-0 Inter star ,LLB 1-2 Athletico ...)


Hapo jana tarehe 4/2/2014 kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore sawa na viwanja vingine vya soka ilichezwa michuano ya wiki ya 8 ya Ligi ya taifa . Mchuano uliyokuwa unasubiri kwa hamu ni ule uliyo zipambanisha Timu pinzani . Mchuano kati ya timu hizo mbili uliwakusanya Washabiki wengi , wapenzi na wadau wa soka , hali ambayo siku nyingi ilikuwa haishughudiwi nchini . Vital'o Fc ambayo iliwapoteza Wachezaji wasiokuwa wadogo baadhi yao wakiwa wameuzikana nje ya nchi na wengine wakiwa wamejiunga na mpinzani wao Inter Star nikizungumzia wachezaji kama DEO NDAYISHIMIYE , NKURIKIYE LEOPOLD KAYA , MICHEL GIRUKWISHAKA na NKURUNZIZA D'AMOUR , kinyume na hao wa Vital'o Fc timu ya Inter star inayo ongozwa na Mh mbunge wa Rumonge KARENGA RAMADHAN imejizatiti vile vile wachezaji kama CHENE MOHSIN , POUTCHOU DEGUERRE , NDUWIMANA SAIDI TAMAA . Kwa upande wa Vital'o Fc kinyume na MIAMI MBAKIYE BABY , JOHN GIRUKWISHAKA , IDDY DJUMAPILI , ABDALLAH MASSOUD , wengi wao ni wapya nikizungumzia kama Wachezaji wa 3 MOUSSA MOSSI HADJ , Kipa OMAR ,na Ballack kutoka kwenye Klabu ya Flambeau de l'Est , Muyaga kutoka kwenye Academie tchite , Zola kutoka Inter star  ndio walijiunga na Klabu hiyo mwaka huu . Fahamu ya kuwa mchuano wao ulimalizika kwa sare ya tasa yakutofungana 0-0 , na Vital'o Fc imesalia kwenye kileleni...

Haya ndio matokeo ya Wiki ya 8 ligi ya Taifa :
---------------------------------------------------------------

Vital’O FC - Inter Stars / Prince Louis Rwagasore , saa Kumi ( 16h ).

LLB Academic 1-2 Athletico Olympic / Prince Louis Rwagasore , saa nane ( 14h ).

Flamengo FC 1-1Royal FC / Buterere ,saa nane ( 14h ).

Muzinga FC 1-1 Volontaires FC / Buterere ,saa Kumi ( 16h ).

Le Messager Ngozi 2-1 Espoir FC / Gatumba ,saa kumi ( 15h ).

Fahamu vile vile ya kuwa Flambeau de l'Est na Academie Tchite hazikucheza kulingana na maandalizi ya kombe la Klabu bingwa flambeau de l'Est yaweza kusafiri Jumaa-tano hii kuelekea Congo-Brazzaville na Academie Tchite safari yake ikiwa imepangwa hapo kesho alkhamis ambao wao wataelekea nchini Rwanda kumenyana na AS KIGALI ya Rwanda . 

Tukizungumzia kandanda nchini uingereza ni  kuwa Mkufunzi Laudrup wa Swansea alifutwa kazi na  klabu hiyo ,taarifa hizo zinajiri siku moja tu baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo Huw Jenkins kupuuzilia mbali tetesi kuwa walikuwa wamezungumzia mustakabali wa Laudrup. Uvumi ulikuwa umesambaa kuhusu hatma ya Laudrup baada ya Swansea kushindwa kwa mabao 2-0 dhidi ya West Ham Jumamosi iliyopita.

Hiyo ilikuwa mara ya sita timu hiyo kupoteza katika mechi nane za Ligii kuu ya Uingereza na kuiacha na alama mbili tu juu ya timu ambazo zitateremshwa katika ligii hiyo.

Monk alikuwa amepigiwa debe kuchukua nafasi hiyo ikiwa mojawapo ya njia za kuboresha kikosi hicho.                                                 


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire