vendredi 7 février 2014

Nyimbo mpya ya Big Farious *what's my name * feat Chany Queen iko tayari ,soma mistari aliyo imba kwenye pini hiyo...

Leo hii usiku mida ya saa mbili ndipo MUGANI DESIRE a.k.a Big Fizzo ameiweka hadharani nyimbo yake mpya *Whats my name * featuring CHANY QUEEN aliyo rikodia Technolojia sounds pamoja nae Docta Jack na A Tizo . Tukiwa tunamuhoji kuhusikana na pini hiyo ambayo ina ujumbe mzito mno alitujibu mengi nakutufahamisha mengi kuhuskina na ratiba ya Tamasha na mengineyo :
Pichani : Fizzo pamoja na Sony Kabu Cherche kabu trouve...

Fizzo :" Nimeamuwa kuichia hadharani pini yangu mpya niliyomshirikisha Chany Queen , zipo nyimbo 3 kuna * best friends , Yahaya na Whats my name najuwa ni nyimbo itakayo wa touch wengi , mimi kama msanii kimbilio langu ni mziki , ninapokuwa na raha ao karaha , kulikuwepo maneneo mengi na hadi mdaa huu yapo , nimetupa jiwe gizani,sijamlenga mtu yule litakalo mgusa basi kimpango wake . Sijatangaza bifu na mtu , najiamini kivyangu ,mimi najisifu nikisema nimeanza kitambo,kwenye game hili nimeanza kitambo , eshima ni kitu cha lazima na chabure . Inakuwa siyo vizuri japo una pesa ,dawa ya ubisho ni kuwa bisho zaidi . Baada ya hii apa ntatengeneza nyingine inakayo julikana kwa jina la * JAJA* , hii apa ni kama whats my name namba 2 ila yenyewe nitakuwa namuenzi Mzee wangu ambae kisha tutoka kitambo , nikama namuenzi vile namfahamisha maswali magumu ambayo yamenikabili kwa mdaa huu . Kuhusu beef nawaweka watu ulimwengu kuwa sina beef na yeyote ,wengi wanazungumzakuhusu lolilo na Franck Duniano ,kiukweli sijuwi nini kwa upande wa hawa wawili . Natangaza live , Lolilo kama nimewahi kukukoseya naomba samahani  , Franck ni rapa mzuri tena anaweza , na kama tulikuweka kwenye Kundi la Wanajeshi ni kwakuwa unaweza ,endelea kazi yako ,nilikuwa nakuamini na bado kwasasa nakuamini ,kama unahitaji kutoka kwenye kundi ni ruhsa yako ,usitaki kutoka kwa beef , nakusihi uendeleye na uko na ruhsa yakutoka na wende unapotaka . Kuhusu Wanajeshi ni kuwa tuko busy sana kila mtu anafanya za kwake ,wakae mkao wa kula ivi karibuni tutafanya mambo makubwa . Tarehe 8/February/2014 niko na Show Rumonge pamoja nae T Max . Tarehe 14 February siku ya wapendanao ntakuwa Archipel pamoja na wanangu Sat B , Black G , na Franck g80 . Vile vile watu wa Dubai mjiandae hapo tarehe 15/February/2014 . Lakufahamu lingine ni kuwa FIZZO ni mmoja kati ya Wasanii ambao wamepewa shavu na Kampuni ya IKOH Multiservice , amepewa shavu ya nyimbo ambayo imeingia tayari kwenye compilation ya Volume 1 ya YOU'LL LOVE CHANGE'S . Jana ndipo alikuwa studio na tayari kurikodi pini hiyo chini ya ufundi wa BOTCHUM ."

Ukitaka kuskiliza fool interview niliyofanya na Big Farious jiunge na link hii : www.radioburundibwiza.com

1 commentaire: