Wawili hao wamekutana leo katika mazoezi ya kikosi chao cha Real Madrid.Bale amejiunga na Madrid akitokea Tottenham kwa dau la pauni milioni 86 ambalo ni ghali zaidi na linazidi lile la Ronaldo aliyejiunga na timu hiyo kwa pauni milioni 80 akitokea Man United.
Wawili hao walikutana na kubadilishana mawazo kabla ya kwenda kubadilisha nguo na kuanza mazoezi.
Baada ya kukutana na Ronaldo, Bale aliendelea kuwasalimia wachezaji wengine pamoja na wachezaji pia memba wa benchi la ufundi akiwemo kocha msaidizi, Zinedine Zidane.Baada ya hapo alijiumuika na wendake katika mazoezi ya mechi ya Jumamosi jioni ya La Liga dhidi ya Villarreal ambayo anatajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye La Liga. Ifahamike vile vile ya kuwa Jezi za kiungo mpya wa Arsenal, Mesut Ozil zimeuzwa zaidi England kuliko za Gareth Bale ambaye amejiunga Real Madrid kwa uhamisho wenye rekodi mpya ya pauni milioni 86.Pamoja na kuwa na rekodi ya uhamisho lakini uchunguzi umeonyesha kila jezi moja ya Bale iliyouzwa kwenye duka la jezi, imeuzwa na tano za Ozil ambaye ametoka Madrid na kujiunga na Arsenal . Jezi za Bale zimeonekana kutokuwa na mvuto wa juu sana na wauzaji wameeleza kwamba zimezidiwa hata na Neymar ambaye hivi karibuni alijiunga na Barcelona akitokea Santos ya kwao Brazil. Kivutio zaidi wawili hao, wote wanavaa jezi namba 11. Lakini Ozil aliondoka Madrid akiwa anavaa jezi namba 10..
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire