mercredi 9 janvier 2013

Amidou Hassan: "Kwanini Inanga music Awards 2012 ? "



Habari za saa hizi wapendwa wa blog hii ya kujuzana mengi ya nyumbani kupitia utamaduni na michezo,yapata sasa miaka 6 nikiwa Mtangazaji kwenye kituo cha redio ya hapa nyumbani Burundi inajulikana kama 'Radio Culture'.Mwaka 2006 nilipo oredheshwa kwenye program ya vipindi niliombwa kuchagua kipindi kipi naweza nikaendesha,sikusita kusema 'Buja beat',kipindi hicho nakumbuka Wasanii wengi wa Bujumbura ndio walikuwa wanafanya vizuri sana kwa upande wa mziki,ila badaa ya mwaka kutokana na safari nilizo kuwa na fanya Mikoani niliguswa sana na vipaji vya Wasanii wa pande za Mikoani,mwaka 2007 nikawa sina ujanja wakugeuza muelekeo waku promote Wasanii wa Bujumbura tu,ikanipelekea moja kwa moja kugeuza nakuita kipindi 'Burundi beat', jina hilo kilikonga nyoo za Wapenzi wa mziki nchini Burundi kilikuwa mara moja kwa wiki,kutokana na maombi ya wapenzi wa mziki wa Burundi wakati 'Radio culture'ilikuwa ikisheherekea mika 10 yatoka ilishimamisha mizizi yake Burundi,Mkurugenzi akawa ameamuwa kipindi ico kiwe kinapita mara 2 kwa wiki,ilikuja kuwa hivo,wakati huo ilikuwa mwaka 2007,ikawa ivo hadi mwaka 2009.Kuanzia mwaka 2010 ambapo nilichukuwa jukukumu yakupanuka zaidi hadi kujiusisha na swali nzima lakuwa na andika kupitia internet,kipindi ico nakumbuka nilikuwa nikipata habari yeyote mpya inausu mziki na wanamziki lazima ni iweke hewani,ilikuwa kama kujifurahisha vile,nakumbuka niliunda hata kakundi flani (Group) iliokuwa inaitwa 'burundi beat' baadhi yenu mnakafamu ila ubovu wa bahati wanaopinga maendeleo yatasnia ya mziki nchini walikafuta,ila ' umoja ni nguvu' inazidi kutupa nguvu zakuzidi kujikwamuwa nakutumika vyakutosha ili malengo yetu siku moja tuyafikie.Kwenye kakundi hako ka marafiki kupitia ukurasa wa kijamii wa facebook nilikuwa wiki kwa wiki naweka hewani TOP 10 ya nyimbo ka;i za wiki,kitu ambacho wengi hasa hasa wapenzi wa mziki wa Burundi walikuwa wanafurahishwa nacho ila kasoro ikawa ni maandishi njo wanaona ila nyimbo hawapati na fasi yakuziskilizia. Ilifkia hadi wakati kutokana na wepenzi kua wengi na baadhi yao kusisitiza kuwa wanataka wawe wanaziskia. 2011 mwanzoni mwanzoni nikapokea sim ya Msanii Mkomboz akanambia kuwa kuna jamaa flani anaishi Arizona/Phoenix anahitaji Mtangazaji ambae anao uwezo wakuhoji na video hio ipeperushwe moja  kwa moja kupitia mitandao ya internet,kipindi hicho nakumbuka sikujali hata nilipwe nilimkubalia kwani nilianza kuona ndoto yangu inaanza kutimia kwani kile nilichokuwa nakilenga nikuwa muandishi wa habari vile vile kupitia mitandao mikubwa mikubwa ,huo ndio ulikuwa mwanzo wakukutana na Mh Pasteur BAGENZINIKINDI,Manager general wa mtambo mkubwa wakupasha habari kupitia internet "www.greatlakesmix.com na www.indundi.com" (Respect sana kwake kwakunifungulia milango yakujipanua na kutambulika kidogo kama Repoter wa habari za tasnia ya mziki na wanamuziki, utamaduni na michezo sana sana mpira wa miguu wa Burundi),mwaka 2011 nilikuwa Mtangazaji wa kwanza presenter kuamuwa kucheza kwenye vipindi vyangu nyimbo za burundi pekee yake,atuwa hio ilini[pa nafasi nyeti yakupongezwa hadi kujinyakulia tunzo 3 muhimu nchini kama Best Journalist of the year (Akeza Awards,Ten in one birashoboka mashindano yalio andaliwa na KIDUM,bila kusahau Big talent ya The Cousins Awards).Ilinipa nguvu zaidi hadi kufkiria mwaka 2012 niwe japo na blog ili niendelee,hata siku moja ikifkia niwe na site web yangu binafsi.Sikukawia sana kwani mwishoni mwa mwezi wa 12 ndipo niliamuwa ku unda blog yangu iliochukuwa jina la "burundibeat".Nikawa nimeamuwa kama ilivyokuwa kwenye mipango yangu siku moja nifanyage kitu kidogo ila muhimu kwa kuonyesha sura nzuri ya nchi yetu ulimwengu,nikasoma jina lipi naweza nikatambulisha vyema nchi yangu,nikaona ulimwenguni kila nchi inakuwaga na nembo ao kitu kinacho watambulisha,nikaona 'Inanga' inaweza kuwa moja wapo,na ndo kwa maana hio...Baada tutawambieni kwanini tuliwagawanya wasanii kwenye ma categories tofauti tofauti tumetizama nini,na kwanini tuwaweke watangazaji,redio,wa Producers na wengineo.mkao wa kula mtaelewa...

-Shukran kwa wale wote wanaozidi ku utowa mchango wao wafikra nakuzidi kunipa nguvu na ku support idea hii...

N.B: Ikiwa kuna fikra ao maoni karibuni kwenye page yetu ya facebook...(Burundi beat Fans page)

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire