jeudi 16 janvier 2014

HALLELUYA FC : Muheshimiwa Raisi Pierre NKURUNZIZA ateuliwa mchezaji bora na mfungaji bora wa mwaka 2013.

Muheshimiwa Raisi Wa Burundi Pierre NKURUNZIZA.
Mwaka 2013 umemalizika , mwaka mpya wa 2014 umeanza tayari na leo una siku 16, kwa upande wa Jopo nzima la ufundi wa Timu ya Halleluya  ni muda muafaka kwa upande wa Timu inayo ongozwa na Raisi wa Burundi na Timu nzima kuweka bayana matokeo (Rapport) ya mwaka mzima uliyomalizika . Jumla ya Mikoa 11 ya Tarafa mbali mbali za Burundi zilichezwa match zakudumisha amani , maridhiano , upendo kati ya timu ya Halleluya na timu hizo  .
Mh Raisi akila pozi na mpira kichwani...
Kama ilivyokuwa kawaida kwa upande wa Raisi wa Burundi ni kukutanisha Raia pamoja kupitia shughuli zakujitoleya (Travaux Communautaires) asubuhi , shughuli hizo zikiwa ni zakusafisha nchi na kujenga mazingira mazuri , baada ya hapo jioni ndipo Raisi huwa anakutana na raia uwanjani . Ni moja kati ya mfano hai kwa wengine Viongozi Ulimwenguni kufkiriya kwani unaboresha secta ya kuweka nchi kwenye mazingira ya usafi na baadae kujenga mwili kwa afya njema kwa upande wawale ambao wanacheza michuano hiyo .

Pichani : Saleh akiwa na Captain PAUL.
Raisi wa Burundi , mmoja kati ya Viongozi bora Ulimwenguni ambae mara kwa mara anakuwa karibu na raia kwa kutekeleza shughuli hizo muhimu kwa upande wa maendeleo wa nchi ya Burundi . Mwaka 2013 kwa upande wa Soka , timu ya Halleluya iliyowakusanyisha kwa kipande kikubwa Wachezaji waliyoandika historia ya mpira Burundi , barani afrika na Ulimwenguni kote hususani kama Kizigenza mwenyewe wa Timu Peter NKURUNZIZA aliwahi miaka ya nyuma kuipa mafunzo klabu ya UNION SPORTING, kama asilimiya 30 ya Wachezaji wanaocheza kwenye Timu hiyo ni wale ambao aliewapa mafunzo alipokuwa akisoma kwenye Chuo kikuu cha taifa . Kati ya hao , wengi wao walipata matunda miaka iliyofwata nikizungumziya kama Nahodha (Capitaine) NSENGIYUMVA PAUL aliye tamba miaka ya nyuma akiwa kama Nahodha miaka minane (8) wa Timu ya A.P.R na Amavubi ya Rwanda , MALA IBRAHIM alietamba kwa mafunzo mazuri aliyopata kupitiya Mkufunzi wake Raisi akaichezeya Union Sporting hadi ku uzikana kwake kwenye klabu ya Vital'o Fc iliyomlazimu kwenda na Djuma Mossi aliekuja kuwa chombo muhimu sana kwa Taifa yake na Vital'o Fc kwa ujumla .
Pichani : Dibwe , Mala Ibrahim na Willy.
 Wapo wengi kama DIBWE , METOUCELA ambae kwa sasa anacheza akiwa Pastor . Wachezaji wanaocheza kwenye Timu ya Halleluya kama nilivyozungumziya hapo juu wengi wao walipata mafunzo kwa Muheshimiwa Raisi na Wengine bahati mbaya yaliyapata pengine ila miaka yao hiyo wali itumiya vizuri kwakuipeperusha bendera ya nchi yao juu . MALICK JABIR aliye wika sana hadi kuwekwa kwenye vitabu , INDELE aliecheza hadi kwenye klabu kubwa kubwa za Afrika ya Kusini na Ulaya , ABUDI BERNARD aliechezeya hadi kwenye Timu ya OBWASSIGWA ya Ghana , KAKENGE aliyefika hadi Kombe la Dunia na INTAMBA MURUGAMBA mwaka 1995 , MNYONGE CHIEF, SIMBA , Nahodha wa zamani JAMAL waliwika sana nchini Rwanda kwenye Timu kama Panthère , Kiyovu Sports...
Pichani : Elengesa na Abudi...

Kinyume na hao pako wengine kama Mh Col. Manaleks , SITA , Afande AMADI, ALEXIS , HASSAN BIGIRIMANA , RAMADHAN, EDDY , ALEXIS, FELICIEN , ARCADE , RICHARD'S , DIOMEDE , ERIC KIDAMAGI , MUHAMAD , MTAMA , WAINA KAPA , MWARABU , MAULIDI , SALEH , EDDY , BULENGE , WILLY , KABEZA , ALLY KING KONG (Kipa) , AMIDOU HASSAN (Mchezaji mwenye umri mdogo) CHADRACK  na wengineo... Kwa muda huu Timu ya Halleluya inapewa mafunzo na Djuma MSOMA aliekuwa Kiongozi wa Union Sporting kipindi Mh Raisi alikuwa Mkufunzi wa Union Sporting.
Pichani : Willy , Chadrack , Aimee Nzohabonayo na Waina.

Kinacho leta faraja ni kuwa toka mwaka 2004 Raisi wa Burundi akiwa na wachezaji hao  anawaweka kwenye ngazi moja na pamoja wanafanya vizuri kwenye jumla ya michuano yote wanayocheza kwenye sehemu mbali mbali nchini .
Pichani : Mnyonge , Indele , Mwarabu , Eric Kidamagi,Malick Jabir , Dibwe...

Fahamu ya kuwa :

. Kati ya michuano  28 iliyochezwa , ilifunga bao 116 . ( 28 matchs = 116 buts ) .

. Mfungaji bora :  - Mh Raisi PETER NKURUNZIZA : 39
                           - Captain Paul : 37
                           - Eddy : 14
                           - Alexis : 13
                           - Mnyonge : 7
                           - Simba  : 6
. Mchezaji bora baada ya uchunguzi wa kina aliteuliwa  Mh Raisi wa Burundi Peter NKURUNZIZA .
Désiré Hatungimana akimsalimu Mh Raisi (Moja kati ya match iliyosisimuwa sana mwaka 2013)
Hii hapa ndio Report ( Bilan ) ya mwaka wote wa 2013 :

NGOZI : 

. LYCÉE GWABIRIRO 3 - 10 HALLELUYA FC ( Mh Raisi goli 5 , Mala Ibrahim 1 , Aimée Nzohabonayo 2 , Saleh 1 na Captain Paul 1)

. (Fonctionnaires de Mwumba )  WATUMISHI WA MWUMBA 1 -5 HALLELUYA FC (Chadrack 1 , Captain Paul 3 na Saleh 1 )

GITEGA :

. LYCÉE GISHUBI 1 - 3 HALLELUYA FC ( Mala Ibrahim1 , Simba1 na Saleh 1)

. KOMINE GIHETA 2 - 4 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 2 ,Captain Paul 2)

KARUZI :

.YOUNG STAR 1 - HALLELUYA FC3 (Alexis 2 , Captain Paul 1)

. KOMINE TANGARA 1 -5 HALLELUYA FC (Alexis 2 , Eddy 1 na Captain Paul 2 )

. KOMINE MWUMBA 1 - 4 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 2 na Captain Paul 2)

RUTANA :

. KOMINE BUKEMBA 2 - 7 HALLELUYA FC ( Eddy 3 , Alexis 1 , Captain Paul 1 na Mh Raisi 2 )

. INTSINZI FC 0 - 5 HALLELUYA ( Mnyonge 1 , Alexis 1 , Captain Paul1 na Mh Raisi 2 )

KIRUNDO :

. KOMINE KIRUNDO 2 - 3 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 1 , Alexis 1 na Captain Paul 1 )

. FC LEOPARD 2 - 4 HALLELUYA ( Captain Paul 3 na SIMBA 1 )

. ABAWIGEZE FC 1 - 2 HALLELUYA 2 ( Mh Raisi 2)

* GITEGA :

. KOMINE GISHUBI 3 - 4 HALLELUYA FC (Mh Raisi 2 na Captain Paul 2 )

. KOMINE KIBIMBA 3 - 4 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 2 , Captain Paul 1 na Alexis 1)

 RUYIGI :

. KOMINE KINYINYA 1 - 7 HALLELUYA FC ( Jamal 1 , Eddy 1 , Captain Paul 1 na Mh Raisi 4)

. KOMINE NYABITSINDA 1 - 6 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 3 , Captain Paul 1 , Mnyonge 1 na Alexis 1 )

MAKAMBA :

. ISAMBWE 0 - 6 HALLELUYA Fc (Chadrack 1, Mnyonge 2 na Mh Raisi 3)

. NYABIGINA 0 - 1 HALLELUYA FC ( Captain Paul 1 )

CANKUZO :

 . KOMINE MISHIHA 2 -  4 HALLELUYA ( Mh Raisi 2 , Captain Paul 2 )

* NGOZI

. KOMINE TANGARA 1 - 4 HALLELUYA FC ( Captain Paul 2 na Eddy 2 )

. KOMINE KIBIMBA 1 - 4 HALLELUYA ( Rama 1 , Eddy 1 , Captain Paul 1 na Mala Ibrahim 1 )

KAYANZA : 

. KOMINE GAHOMBO 2 - 5 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 1 , Eddy 3  na Mnyonge 1 )

. KOMINE KABARORE 1 - 2 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 1 na Eddy 1)

** NGOZI :

. KOMINE MWUMBA 1 - 5 HALLELUYA FC ( Captain Paul 1 , Mh Raisi 2 , Alexis 1 na Eddy 1 )

MURAMVYA :

. KOMINE BUKEYE 3 - 7 HALLELUYA ( Eddy 1 , Alexis 1 , Mh Raisi 1 , Simba 1 ,Mnyonge 1 na Captain Paul 2)

. KOMINE KIGANDA 0 - 4 HALLELUYA FC (Mh Raisi 1 , Willy 1 , Simba 1 na Captain Paul 1 )

. KOMINE MURAMVYA 1 - 4 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 1 , Alexis 1 , Simba 1 na Captain Paul 1 )

MWARO :

. KOMINE NYABIHANGA 2 - 3 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 1 na Captain Paul 2 )

. LYCÉE MWARO 1 - 3 HALLELUYA (Mh Raisi 2 na Captain Paul 1 )

. JAGUAR FC 1 - 6 HALLELUYA FC ( Mh Raisi 2 , Alexis 2 , Mnyonge 1 na Ramadhan 1 )

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire