vendredi 10 janvier 2014

CHAN 2014 : INTAMBA MURUGAMBA wanasafiri saa nane usiku tarehe 11/1/2014 kuelekeya South africa.

Intamba[1]
Intamba Murugamba wakiwa mazoezini
Baada ya kuwa kipenga kitapulizwa ifikapo kesho tarehe 11/1/2014 nchini Africa ya kusini , Burundi yao kutokana na uwezo wake mdogo inatimba usiku wa leo , yaani saa nane usiku( 2h du matin)  kuelekeya Polokwane itakapochukuwa kambi nakuchuana mechi 3 za duru ya mtoano kwenye kundi la D ambapo zinajikuta timu za DRC , Mauritania na Gabon . Kwa upande wa ufundi wa timu ya taifa na Saido kutokeya nchini Polond akiwa anajinowa nao pamoja wanasema :

 - Réverien NDIKURIYO ( Kiongozi wa FFB):" Timu ya taifa iko sawa , walipata na fasi nzuri yakujinowa kwa michuano yakujipima nguvu walipokuwa Kenya kwenye kinyanganyiro cha CECAFA , kinachobaki tu ni wao kujituma nakufahamu kuwa wanaiwakilisha taifa,kila la kheri kwao..."

- Amars NIYONGABO :"Mes joueurs sont capables d’affronter n’importe quelle équipe. Ils ont éliminé tour à tour le Kenya, le Soudan, certains clubs de la RD Congo, le Rwanda,… Rien ne les empêchera d’aller loin ».

Akimaanisha :" Wachezaji wangu wako tayari kumenyena na timu yeyote ile . Walizitowa mashindanoni timu ya kenya, Sudan , timu tofauti za DRC , Rwanda,...haitowakataza kuendelea mbele."

- Saido NTIBAZONKIZA anaye fanya mazoezi na timu hiyo ya taifa :" Ukosefu ya match nyingi zakujipima nguvu inaweza kuiponza timu yetu ya taifa. ila hiyo haito nikata nguvu yakuwapa sapoti yangu watakapokuwa tayari South africa."

Fahamu ya kuwa kuchelewa kwa Burundi kujielekeza kwenye ardhi ya mandela nikutokana na bajeti ndogo ya Serekali kwani Tume ya maandalizi inaanza kugharamiya Timu zote siku 3 kabla ya kipenge kupulizwa . Kinyume na wachezaji 23 tuliyokutajiya siku za nyuma , watakao shiriki kwenye msafara huo ni pamoja na wakufunzi watatu ( Naseem Lofty , Olivier Mutombola na Amars) bila kusahau viongozi mbali mbali kutoka kwenye Shirikisho la Soka nchini na Wizara ya Vijana, Michezo na Utamaduni, na Jopo la waganga bila kusahau Mtangazaji . BB inawatakiya kila la kheri kwenye mashindano hayo.
 

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire