jeudi 21 mars 2013

Kenya : PREZZO KUPIGA SHOW DAR ES SALAAM APRIL 5

Msanii kutoka 254 CMB Prezzo, anatarajia kufanya makamuzi ndani ya New Maisha Club - Dar es Salaam. Show hiyo inatarajia kufanyika ijumaa tarehe 5 April 2013. Prezzo atakuwa pamoja na wasanii wa hapa nyumbani watakao panda nae stage moja akiwemo Feza, Stereo, Shosteez na wengine surprise kwa mashabaki wa muziki wa kizazi kipya. Hii ni mara ya kwanza kwa Prezzo kukamua ndani ya Club.
Prezzo ni msanii ambaye anafanya vizuri katika game, ladha fresh za single zake 2 mpya alizoziachia hivi karibuni akiwa moja ame - dedicate kwa marehemu mchumba wake Goldie ambayo inaitwa "Naija Girl". na nyingine ni 'Liqher' ambao imekuwa gumzo Afrika Mashariki na Kati, zitasikika kwa mara ya kwanza live siku hiyo. Prezzo siku hadi siku anajizolea umaarufu mkubwa sana bara la Afrika hasa baada ya ushiriki wake katika jumba la Big Brother Star Game 2012 na kuibuka kinara namba 2 na kutuwakilisha Afrika Mashariki.Msanii ambaye amekuwa gumzo na stori kwa mashabiki mbalimbali ambaye juu ya muonekano wake kuwa wa kipekee (swagga) . Na siku zote amekuwa mtu wa watu. Prezzo amefanya kazi kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali akiwemo AY kutoka Tanzania, Wyre, Bamboo, Naziz na wengine kibao. Na nyimbo zake kushika chat katika vyombo mbalimbali vya habari,nyimbo kama Ma Fans, Naleta Action, Ma City Ma Town, Tupendane, For Sure For Shizzle na nyinginezo.
Basi kwa mashabaki wa Prezzo atakuwepo Liveeeee in Dar...Dont miss out...

Source:Bestizzo.com

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire