Pichani :Pique na Shakira... |
Mwanamuziki maarufu wa kike, Shakira na kipenzi chake, beki wa Barcelona, Gerard Pique wamezidi kuonyesha kuwa penzi lao liko hai baada ya kujitokeza katika mechi ya mpira wa kikapu.
Mechi hiyo, timu ya Barcelona ilikuwa inacheza dhidi ya Fenerbahce Ulker Istanbul kwenye Uwanja wa Palau Blaugrana jijini Barcelona. Wawili hao walionekana kuwa karibu na kujadili mambo kadhaa huku mkono wa Shakira ukiwa katika paja la mpenzi wake huo muda wote.Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kwamba wako kwenye mfarakano ndiyo maana siku nyingi hawajaonekana pamojaKutokea tena wakiwa wenye furaha, inaonyesha wazi ni kama jibu la waliokuwa wakieleza kwamba wako katika mtafaruku.
TABU LEY AFARIKI DUNIA
Mkongwe wa muziki wa dansi nchini DR Congo, Tabu Ley amefariki dunia nchini Ubelgiji.
Tabu Ley amefariki nchini humo baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya miaka minne.
Mkongwe huyo ndiye mwazilishi wa miondoko ya Sokous iliyoshika chati na kuwa moja ya aina ya muziki uliopendwa zaidi duniani. Alitamba wakati huo pamoja na mwanamama Mbilia Bel ambaye baadaye alihamia nchini Kenya. Baadhi ya albamu zake kali wakati wa uhai wake ni Tompelo, Babeti Sokous, Tete Nakozonga na Muzina ambayo ilikamata ile mbaya.
Huyu Ndio Mshindi Wa EBSS 2013 :
Mshindi wa shindano la vipaji Epic Bongo Star Search Mwaka 2013 Ni Emmanuel Msuya. Amezawadiwa pesa za KiTanzania Milioni 50 Na Mkataba wa Kurekodi Chini Ya Studio Ya Mj Records
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire