jeudi 12 septembre 2013

Manchester :ROONEY AREJEYA KAZINI...AANZA MAZOEZI RASMI NA FELLAINI.

Aki ingia saloon
Akiondoka zake...
Akitokea Bank


Siku chake kabla ya kuanza kazi, kiungo Marouane Fellaini ameonekana akiingia kwa kinyozi kurekebisha nywele zake. Fellaini ameonekana akiingia kwa kinyozi katika moja ya vitingoji vya jiji la Manchester, baadaye akaingia benki halafu akarudi katika gari lake aina ya Audi. Hali hiyo imeonekana ni yeye kujiandaa kabla ya kuanza kazi katika klabu yake mpya ya Man United aliyojiunga nayo akitokea Everton.

R and R: Rooney spent the international break on holiday in the Algarve
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney yuko tayari kuanza mazoezi kamili na Manchester United akidhamiria kuwa kujiweka fiti kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu, City Jumapili.
Rooney, mwenye umri wa miaka 27, alikuwa akifanya mazoezi na wataalamu wa tiba wa United kwenye Uwanja wa mazoezi wa klabu, Carrington jana na anaonekana kuwa fiti baada ya kuumia kichwa alipogongana na Phil Jones kiasi cha wiki mbili zilizopita.Lakini mshambuliaji huyo United anapewea asilimia 50 kwa 50 kucheza mechi dhidi ya timu ya Manuel Pellegrini, City Uwanja wa Etihad, Septemba 22. 

Wasiwasi: Rooney inafahamika alikuwa anafanya mazoezi kivyake nje ya timu, na David Moyes hayuko tayari kumharakisha kurejea uwanjani Moyes tayari amekubali kumkosa Rooney katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Crystal Palace Ligi Kuu ya England na anatarajiwa kucheza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayer Leverkusen Uwanja wa Old Trafford JUmanne ijayo.
Mchezaji mkubwa pekee aliyesainiwa United ni Marouane Fellaini, mwenye umri wa miaka 25, na anatarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa wiki hii.
Mshambuliaji huyo amecheza kikamilifu mechi moja tu United msimu huu, na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika sare ya 0-0 na Chelsea Uwanja wa Old Trafford.
Alitokea benchi katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Swansea, akitoa mchango wa kupatikana mabao mawili kati ya manne ambayo timu yake ilivuna siku hiyo.
On the mend: Wayne Rooney poses with a fan after recovering from his head injury - he was back in training for the first time on Wednesday
Picha hiyo yupo na shabiki wake,akionekana amepona jeraha.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire