|
B FACE na NJC washindi wawili wa Mkoa wa kayanza. |
Mashindano ya Primusic 2013 yakiwa mwaka huu yameingia kwenye siku yake ya pili yalifanyikia Mkoani Kayanza ambapo mashindano hayo yalifanyika bila kuwepo Tamasha yeyote yauchakachuwaji wa Wasanii mbele ya washabiki.Duru za uhakika kutoka kwenye waandalizi wa mpango mzima wa primusic 2013 wametupa ripoti kuwa washindi wawili walipatikana kwa ujumla ya walioshindana asubuhi ya leo,
GIRUKWISHAKA Boniface wengi wakimuita kwa jina la utani kama
B Face ambae anazo kibindoni pini nyingi na kati ya hizo huwa anashirikiana mara nyingi na
Baby Chou msichana ambae vile vile anafanya vyema kwenye gwaride ya mziki wa hapa nchini.Mungine aliejishindia nakujikatia tiketi yakuingia kwenye robo fainali moja kwa moja ni
NIYONKURU Jean Claude a.k.a NJC ambae hazoweleki sana kwenye ulimwengu wa mziki. Ifahamike ya kuwa siku ya tatu ya mashindano hayo yamepangwa kufanyika Mkoani Ngozi itakuwa ni siku ya Jumaa-mosi (Tarehe 27 July 2013) na Jumaa-pili (Tarehe 28 July 2013) itakuwa Mkoani Kirundo. Mwaka huu ni kuwa mashindano hayo yatakwenda haraka mno kinyume na mwaka jana tukilinganisha na mpangilio ulivyopangwa,mwaka jana ilikuwa washindi wawili wanapo pita wanaingia kwenye ngazi ya mkusanyiko wa Mikoa yakikanda (Régional) ila mwaka huu wanao pita moja kwa moja wanaingia kwenye ngazi ya robo fainali (1/4 final).
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire