mercredi 24 juillet 2013

Primusic 2013: Washindi wawili wa Mkoani Bujumbura Vijijini wamefahamika leo Gatumba...

Golbi & Karim
Asubuhi ya leo kwenye ukumbi wa Cercle nautique ya Bujumbura ndipo mashindano yakuchakachuwa vipaji vya wasanii nchini yalianza yakiwa kwenye mwaka wake wa pili (2eme Edition). Mashindano ambayo yamulikwa kumalizika ifikapo mwezi wa 9. kwa ujumla walikuwa 24 waliojiorodhesha ,ila waliojitokeza walikuwa 20 na kati ya hao wanao jihusisha na uchakachuaji (Membres du Jury) wakawa wamesalia na Wasanii 10 wakiemo :
20 walioshiriki kati ya 24 waliokuwa wamejiorodhesha.

1.NSHIMIRIMANA OLIVIER

2. NIYONGABO OLIVIER a.k.a Golbi

3. NSENGIYUMVA PIERRE

4. AKIMANA KARIM

5. BIGIRIMANA INNOCENT

6. TUYISABE JIMMY

7. HABONIMANA JOHN

8. NSHIMIRIMANA DESIRE

9. UWIMANA PATRICK

10. HAKIZIMANA THIERRY
Ili ndilo gari lnalo raisisha mpango mzima wa Primusic 2013.
Black Snakes walikuwepo na waliridhisha watu.
Rally Joe alikuwepo na alichangamsha watu vyakuridhisha.
T Max alichana,alifoka na akaelimisha waliohudhuria.
Picha ya siku ya leo...
Sat b alishindikizwa na kundi la " Top Dance".
Baadhi ya washabiki waliohudhuria...
Pichani: Arnaud,Alida na Buddy ( Jury )
Jopo la ufundi mitambo likiongozwa na Mshenge...

Kwenye siku yake ya kwanza tarafani Gatumba , walianza nakuwapa fursa wanao unda kundi la Black Snakes , vijana wakali sana kwa upande wakucheza nyimbo tofauti tofauti . Kwa upande wakiufundi na wanao jiusisha na kurekebisha swali nzima la Primusic 2013 ni kuwa,wamebadili mambo mengi kama kwa mfano :

*Animation (Mc) : Mwaka jana ilikuwa MICHOU na MASHOKE ila mwaka huu walipewa shavu CHRISTIAN NSAVYE na ERNEST PABLO BARYUWABO.

*Ambassadeurs (Wabalozi wa mashindano hayo )  : Mwaka jana ilikuwa KIDUM na BIG FIZZO ila mwaka huu walipewa shavu RALLY JOE mshindi wa Primusic 2012 na SAT B. Wameongezwa vile vile Mkomboz, T Max,Masterland  na saidi Brazza. Ila hao wa 4 watakuwa wakionekana kwenye Tamasha

*Medias  : Zilikuwa Radio zakibinafsi za hapa nchini ila mwaka huu wamepania sana kwenye mitandao yaki jamii na vile vile blog yenu hii ilipewa shavu yakufwatilia kwa karibu mashindano yenyewe.

*Prix ( zawadi) : Mwaka jana wa kwanza alipewa milioni 10, ila mwaka huyu wa kwanza atapata milioni 15, na watakao pata tunzo ni wale wote watakao ingia kwenye ngazi ya fainali .Mashindano ya kwanza kwa upande wa Mkoa wa Bujumbura Vijijini yamemalizika na Washindi wawili ambao tayari wameingia moja kwa moja kwenye Robo fainali wamefahamika wakiwemo : AKIMANA KARIM ,ni mmoja kati ya vijana wanao unda kundi la "Cat Sounds" na NIYONGABO OLIVIER a.k.a Golbi, msanii ambae tayari ananyimbo yake moja inayosimama najina la "ABARUNDI". Kinyume na mashindano ya hao 10 bora kwenye Mkoa wa Buja Rural , Wabalozi wa mwaka huyu SAT B na RALLY JOE waliwashindikiza  na gwaride ndefu ya burudani nakuweza kuwa acha hoyi washabiki wa pande zile waliokuwepo kwenye uwanja wa mpira uliopokea mashindano hayo . Sat B alionyesha kiwango kikubwa na kila aliekuwepo alifurahishwa nacho kwani alikuja binafsi na kundi la wachezaji toka kwenye kundi la "Top Dance" , vijana ambao walionyesha kuwa wanao uzowefu wa hali ya juu . Matokeo kwa ujumla yalipokelewa na walio hudhuria ila wengi hawakuridhishwa na 1 kati ya wawili hao waliochaguliwa nakuweza kusema kuwa ingelikuwa vyema usahili utakao fwata watangaze mapema vigezo ili watakao shuhudia moja kwa moja kinyume na alama za wachakachuwaji( Jury) na wao pia waridhike na wale wataokuwa wamechaguliwa kwakutowa muono wao. Ifahamike vile vile ya kuwa palikuwepo ulinzi wakutosha jambo lililo furahisha wengi waliokuwepo hapo . Siku ya Jumaa mosi 27/July na Jumaa pili 28/July akipenda Mungu tutakuwa Ngozi na Kirundo,matokeo kamili mtayapata hapa hapa. Fwatilia karibu mashindano hayo kupitia blog yenu hii,mengi zaidi yenye kuchunguzwa kwakina mtayapata ...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire