dimanche 28 juillet 2013

Primusic 2013 : Washindi 3 walitambulika leo Mkoani Ngozi...

Pichani : Masterland , Sosthene & Alain Jules Twizere
Baada yakuwatambuwa Washindi kutoka Mikoa ya Bujumbura Vijijini na Kayanza,leo hii ilikuwa ni zamu yakuwafahamu washindi watakao wakilisha Mkoa wa Ngozi,Mkoa ambao mwaka jana uliacha hoyi washabiki wengi wa mziki kulingana na ujuzi wa hali ya juu ambao wanao wanamziki wa pande zile japo yakutengwa na media tofauti za hapa nchini. Jumla ya wasanii 21 waliokuwa walijiorodhesha ,11 ndio walioweza kuwasili kwenye kituo hapo jana nakuweza kushindana kati yao wasanii kumi ndio walipita nakuweza kushindana leo mbele ya umati wa watu waliohudhuria kuja kuona moja kwa moja tamasha yenyewe. Baada ya mashindano hayo malalamiko kwa baadhi ya wasanii walioweza kujiorodhesha yalijitokeza huku baadhi ya waandishi kuandika kupitia ukurasa waki jamii kuwa wameonewa nakutupa lawama kwa waandalizi wa mashindano yenyewe . Duru kutoka Ngozi zinasema kuwa mashindano ndivyo yalipaswa kufanyika kwani wasanii wote waliojiorodhesha tarehe walikuwa tayari wanaifahamu,na kama ilivyokuwa kawaida siku moja kabla lazima wapitiwe kukumbushwa kwa utumiaji wa gari (Road show) na mabango (affiche) kutambazwa kona mbali mbali
Rally-Joe alitimuwa vumbi...
Wasanii 10 waliovuka ngazi ya fainali.

Sat b kama balozi mwaka huyu wa Primusic alikuwepo.
washabiki walikuwa wengi.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire