mercredi 3 juillet 2013

Papiss Cisse: Siko tayari kukiuka sheria za dini ya Kiislamu kwa ajili ya soka.

(TaylorSteven ) Jezi inayo kataliwa na Wachezaji hao...

Klabu ya New Castle inayosakata kabumbu kwenye ligi ya primia nchini Uingereza, ambayo katikati ya msimu uliopita ilimpoteza mshambuliaji wake mahiri Demba Ba ambaye alitimkia klabu ya Chelsea ya mjini London, hivi sasa kuna hatihati inaweza kumpoteza mchezaji wake mwingine mashuhuri Papiss Cisse raia wa Senegal, baada ya kukataa kuvaa jezi ya timu hiyo yenye tangazo la WONGA.COM, wadhamini wapya wa klabu hiyo msimu ujao. Papiss Cisse ni muumini safi wa dini tukufu ya Kiislamu na aliwaambia viongozi wa klabu hiyo juu ya kutokuwa tayari kwenda kinyume cha maadili ya dini yake kwa kutangaza biashara za kampuni hiyo ya mikopo. Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, waumini wa dini hiyo hawaruhusiwi kunufaika au kujinufaisha na riba kutoka kwa mtu mwingine. Wachezaji wengine Waislamu wa klabu hiyo ya New Castle ambao ni Waislamu kama vile, Cheick Tiote na Hatem Ben Arfa, huenda nao wakachukua uamuzi kama huo wa Cisse wa kugomea jezi hizo. Hivi sasa klabu hiyo iko njia panda, kwani haiko tayari kumuacha mchezaji huyo inayomtegemea atimkie klabu nyingine, na kuna uwezekano mkubwa kwa klabu hiyo kufanya kama ilivyokuwa kwa Frederick Kanoute raia wa Mali aliyegoma kuvaa jezi yenye nembo ya tovuti ya 888.com alipokuwa akiichezea Seville ya Uhispania miaka kadhaa iliyopita, kwa sababu ya kamari.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire