jeudi 28 février 2013

Member ameteuliwa kuwa muwakilishi wa SICA kwenye Jumuia ya Africa Mashariki...

Mwanamuziki wa zamani na kiongozi wa baraza la wanamuziki nchini Burundi Mh BRUNO SIMBAVIMBERE alias MEMBER ndie ameteuliwa kuwa muwakilishi wa SICA (Mashindano ya muziki nayofanyika kila mwaka nchini BENIN ). Ameteuliwa kwenye nafasi hio ambayo ni muhimu sana kwa muziki wetu ambao umeanza kutapaka kwenye sehemu mbali mbali ulimwenguni . Member ameridhishwa na hatuwa hio na akusita kusema kuwa :" Akanyoni katagurutse ni kamenya iyo bweze' akimaanisha ( Mguu uliotoka umebarikiwa), hio ni baada ya kushirikiana na Msanii Emelance Emy NIWIZERE aliesafiri mwaka jana na kuibuka na ushindi wa tunzo la Video bora ( Yambogorera ) alipokuwa anaongea na Mtangazaji toka Radio Isanganiro na Ripota wa GLM CHRISTIAN NSAVYE alibainisha kuwa :" Burundi inakubalika na ina sifa kubwa kwa upande wa muziki live kwenye kanda nzima ya East africa na hii ni ituwa kubwa sana kwa nchi ambazo tuko pamoja kwenye kanda ya Afrika Mashariki." Ikumbukwe ya kwamba MEMBER anaujuzi wa hali ya juu kwa upande wa muziki,alikuwa kwenye kikundi cha zamani cha ORCHESTRE NTAHANGWA RIVER ya BAHAGA Prosper mwaka 1983 na mwaka 1985 akawa ameungana na Wasanii mahiri waliojijengea sifa kemu kemu kama Tchanjo Amissi , Africa Nova ...Baada ya mchafuko wa vita uliotanda nchini,aliamuwa ku unda kundi lake 'LION BAND' ambalo nia kubwa ilikuwa nikuzagaza ujumbe wa amani na upendo nchini...

*Kumbukumbu za ambao walishashiriki:
-------------------------------------------------------
2009: Steven SOGO ( Nyimbo bora 'Il est beau mon pays' )
2010 :Albert KULU
2011 : Shazzy Cool Harera
2012 : Emelance Emy NIWIZERE ( Video bora 'Yambogorera' ) 

1 commentaire:

  1. Toutes mes felicitations mon cher Member. Il est vrai que la musique burundaise gagne du terrain dans l'arene international. Dommage que dans the East African Community, cette musique se limite sur les chansons de Kidumu. Je suis sur que des personnes comme Gilbert Ndakoze, Ngabo Leonce etc... ont des styles que l'Afrique de l'Est ignore. Des chansons burundaises dans le style Jazz, Blues, etc...
    Par exemple, the East African Radio de Dar es Salaam se limite sur les 3 pays sedentaires de l'Afrique de l'Est le Kenya, la Tanzanie et l'Ouganda. Il faut secouer les responsables Burundais au sein de la communaute pour qu'ils en parlent. Merci et a tres bientot.

    RépondreSupprimer