dimanche 20 janvier 2013

CAN 2013: DRC 2-2 GHANA (mzizi wakukosa ma bao ulikatwa leo hii)Pichani : Mputu Maby Tresor na Asamoah...
Baada ya match 2 za jana kumalizika bila kupatikana bao(South africa 0-0 Cap Vert)na (Maroc 0-0 Angola),leo hii mzizi wa fitna umekatwa baada ya timu 2 vigogo barani Africa kukutana,nazo zikiwa ni pamoja na DRC & GHANA.Timu zote 2 ziliridhika na sare ya bao 2 kwa 2.Match hio iliochezwa kwenye uwanja wa Port Elisabeth ambao haukujaa sana kama ilivyokuwa inasubiriwa na halaiki ya wapenzi wa mpira wa miguu,hususani mashabiki wa Jamuhuru ya Democratia ya Congo,na timu ya Ghana.Mchezo huo ulikuwa na mvuto wa hali yajuu,kipindi cha kwanza kimetawaliwa na wachezaji wa Ghana hadi kupata bao 2 zilizofungwa na Badu (dakika 40) na (dakika ya 50). Kipindi cha pili vijana wa Mfaransa Claude le Roy walikuja juu nakuweza kurudisha bao zote mbili zilizofungwa na Mputu Mabi tresor,nahodha wa timu hio kwenye dakika ya 53,na mwenzie Mbokani akasawazisha kipitia mkwaju wa penalti kwenye dakika ya 69.Mchezaji wa PSG Mulumbu alikuwa aipe ushindi DRC kwenye dakika ya 83,ila goalkepeer wa Black Stars Dauda akawa ameokowa.Kwa upande mungine Robert kidiaba alionyesha ubabe wake kwakuokowa mipira 3 ya Asamoah Gyan kwenye dakika ya 71,77 na 94.Tumependa kuwafahamisheni habari hii kwa wale wapenzi wa kandanda na hasa hasa wapenzi wa Leopards ya Congo ikiwa moja kati ya nchi inawakilisha kanda ya maziwa makuu...


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire