mardi 22 janvier 2013

Bubanza: -Mr JOJO:" Tuna ahidi kufanya mengi mazuri huu mwaka wa 2013..."
Blog yenu hii imepata fursa kwenye likizo fupi kutembelea mkoa wa Bubanza nakuitaji kujuwa kipi kinachoendelea kwa upande wa mziki na Wanamuziki pande zile. Kama mnavyofahamu ao pengine mlikuwa hamfahamu Mkoa wa bubanza uko na Studio moja inajulikana kama 'Umuco records' inamilikiwa na mmoja kati ya Wasanii wa pande zile Mr JOJO. Tulipata fursa yakutembelea studio hio na kuyafanya mahojiano madogo kuhusu mpango mzima wa kazi kwenye studio yao na mziki wa Bubanza kwa ujumla. Alitwambia:"Tunakuja na nguvu nyingi sana mwaka huu,yani niko tayari kuyafanya mengi mazuri 2013. mziki wa Burundi lazma tuupe thamani,natoa wito kwa Wasanii wote sana sana wale kutoka pande za Bubanza,Cibitoke na Kayanza Umuco Records ipo kwajili yao." 

Aliongeza nakusema: "Hivi karibuni nafungua branch ya kutengeneza videos yani "Umuco videos" kuna pia na timu itakayojihusisha na kuaanda matamasha ( Concerts) ya ku promote wasanii ambao nitakua nimetumika nao. Mipangilio (Projects) ni mingi kwenye Umuco Entertainment Company,tutazidi kuwajulisha pole pole,jinsi siku zitakazokuwa zinakwenda. " Alimalizia nakutwambia kuwa: "Ki binafsi kama muimbaji, ipo album yangu ya kwanza ma saa 24 cini ya 24 (24h/24h) nimeitoa mwezi wa September,hivi naendelea kuifanyia promotion na videos niko nazitengeneza. Very soon wataziona!! We are ready to rock 2013." Habari ndio hio...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire