Pichani : Rally Joe akiwa na AFISA RAJ B. |
" Inasikitisha kuona Burundi watu wengi hawajaelewa Hiphop ni nini....yani unapomdiss msanii fulani, wanasema eti ni bifu...but as days go by najua mtaelewa tu polepole...Diss sio Bifu jamani...juweni kutafautisha hivyo vitu viwili...na ndo maana mziki hausongi mbele coz wengi hawajaelewa. Thanks! ''
Fahamu ya kuwa wakati mrefu mkali huu wa hip hop anadendelesha maisha yake nchini kenya .
- Hii ndio mistari aliyo iacha hadharani kwa niaba ya T MAX na UNCLE CRAZY GISAZI :
Diss kwa T.Max
Naongea nawe Max coz naona hauna jipya/
bora wende uka-relax kimziki tushakuzika/
ulazwe mahali pema peponi amina/
hauna tena cha kusema kitaani imebaki jina/
una copy na ku-paste alafu unajiita bingwa/
if yu think yu best basi game umeshashindwa/
unajiita mkali wa michano na tuko wengi zaidi yako/
kwa rap sina mfano bisha nikugonge tako/
we unacopy mpaka tungo mpumbavu buni vya kwako/
kuanzia dear chemchem hadi leo uko mistariless/
kwa hili game mi ni mshindi muulize hata prince/
sina u-same na mapimbi mi mkali eversince...
-------------------------------------------------------------------------
Diss kwa Uncle Crazy
(Jibu ya Hatufanani nao) :
Aye yo..Ni kweli hatufanani/
kiongozi na mtawala sera zao hazilingani/
kwanza mi nasuka we una rasta kichwani/
sasa vipi tutafanana mi muislam we mpagani/
sio eti nabana ukiwa soldier mgambo nani/
watu wanaimba vya maana unaboronga hauoni haya/
kama umeshindwa kuchana basi nenda ukaimbe kwaya/
haijalishi we ni gangi mi kwangu nakuona mende/
punguza stimu za bangi la sivyo kashike jembe/
sijitahidi mi naweza rap mpaka unakimbia/
chap chap nakuharibia/
nikiwa kimya jua naitunga sheria/
mi ni kobe we ni ng'ombe basi usije kuvamia/
aaah...kutangulia sio kufika/
ni-battle face to face uone ntavyokufunika/
kwanza staili yako ni gani una-rap au unaongea?/
unadai kuwa hewani dass wassup ushapot
ea/ una vina za kitoto na ndoto zako potofu/ we ni choko mwenye msoto ka sim za China we mbovu/ we ni King wa ma-crazy hauwezi shindana nasi/ hujawaha soldier ewe mbuzi njoo nikulishe nyasi/ mbele ya kusema kwanza chunga wako ulimi/ hatutaki upuuzi tena hivi unachofunza nini?/ chemsha bongo utowe ujumbe sio pumba/ toa matongo uone mbali usije yumba/ Afisa niko shuwa kukosoa kila siku/ funika ntafunua huyu ni usia sio bifu/ twatofautiana staili mistari mpaka hisia/
usiulizi maswali eti wapi nilianzia/ Show gani za mbali unazofanya hatuzioni/
na nani anakukubali unasahau ulibebwa mgongoni/
hauna ukali wowote blaza njoo nikufunze/
umeukonga acha uuote jitokeze nikuburuze......#KINAMA CITY 4 LIFE.
Je! anayosema ni kweli ? Kulikoni kwa Uncle Crazy na T MAX ,wanazungumziya nini ? Tunafwatiliya kwa karibu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire