Karenga Ramadhan |
Leo hii tarehe 16/November/2013 ndipo klabu ya weupe na wausi maarufu kama Inter Star wamefanya uchaguzi wa kamai tendaji mpya yakuiongoza klabu hiyo kwenye misimo 4 ya mbele . Timu hiyo baada yakuongozwa na DEO NGENDAHAYO miaka kadhaa na wengi kulalamika kuwa hawakuyaona mabadiliko yoyote kwa upande wamaendeleo ya timu ndipo kamati tendaji ya klabu hiyo ikaanda uchaguzi na wakawa wameteuliwa :
- KARENGA RAMADHAN : Kiongozi mkuu (Président)
- SERGE : Naibu wake( Vice-Président)
- SABIMANA SHABANI alias Captain ALLY :Naibu kiongozi wa pili (2ème Vice-Président)
- BRUCE MUFUGUTU : Secretaire général.
Baada yakutambulika washindi hao ,ilifahamishwa kuwa uchaguzi wa viongozi wa washabiki nakuipanga kamati tendaji kamili (Comité exécutif ) ni hivi karibuni .
Habari zingine za michezo kwa upande wa kandanda nchini ni kuwa hapo kesho vile vile tutatambuwa mshindi kati ya REVERIEN NDIKURIYO na Mama LYDIA NSEKERA kusimamiya shirikisho la mpira nchini FFB ,tume ya watu wawili kutokeya FIFA tayari wamewasili nchini kufatiliya mpangilio huo.
Vinginevyo timu ya taifa tayari imeshakamilisha kwakuandika waraka wa rambi rambi kwa shirikisho la mpira kwenye kanda ya afrika mashariki na kati maarufu kama CECAFA kujiorodhesha kwenye timu zitakazo wakilisha vikosi vyake kushiriki michuano inayomulikwa kuanza rasmi ifikapo tarehe 27/11/2013 nchini Kenya. Burundi imo kwenye kundi la 2 pamoja na ZAMBIA,TANZANIA na Somalia. Makundi yamepangwa ifwatavyo :
A: Kenya, Ethiopia, Zanzibar na South Sudan
B: Tanzania, Zambia, Burundi na Somalia
C: Uganda, Rwanda, Eritrea na Sudan
Tunawatakiya mafaanikiyo mema.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire