ARAKAZA Mc Arthur |
Arthur akiwa mazoezini South africa kwenye shule la academy Farouk Abrahams. |
Arthur akiweka hewani moja kati ya tunzo aliotwa na timu yake ya Academy. |
kikosi cha Burundi zidi ya Kenya,Arthur ndie alikuwa langoni... |
-AH: Habari yako?
*Arthur: Niko poa sana my brother.
-AH: Umezaliwa wapi,lini ?
*Mc Arthur: Nimezaliwa Burundi,Mkoani Makamba tarehe 29/July/1995
-AH: Tupe kwa muhtasari (kwa ufupi) maisha yako ya mpira.Ulianzia mu timu gani?
*Mc Arthur: Yeah... Nimeanzia mu Aigle noires ya Makamba mwaka wa 2006 ndio naweza sema kuwa nimeanza kuceza mpira rasmi,mwaka 2007 kwa ushirikiano na wachezaji wenza nikizungumzia kwa mfano kama Tambwe Amissi,Rugonumugabo Stefane,Yahya... tulijaliwa kupandisha timu mwaka 2007 kwenye ligue B/Mikoani,mwaka huo huo tukajaliwa kuipandisha tena Ligue A ya taifa,baada ya hapo hatukufanya vizuri tukajikuta tumeshuka daraja. Sikusalia hapo ili nibidi nijifunze ni toke vipi ili ufundi wangu kimpira usifie bure,baada ya hapo nikawa nimesajiliwa na timu ya dara la kwanza (Vital'o fc),kwenye timu hio nilicheza kama michuano 5,nikawa nimepata nafasi nyeti nikionganishiwa na Kiongozi yaani President wangu Mh Reverien kujiunga na shule ya Academy ya makipa wa mpira wa miguu mwaka 2009 mjini Cap Town,nchini South africa tukiwa pamoja na aliekuwa Mkufunzi wa makipa wa timu ya taifa ya Bafana Bafana FAROUK Abrahams . Nilimaliza nae miaka miwili na nusu,nakumbuka wakati huo kuwa nilipiga hatuwa yakuridhisha kwani kwenye timu ya Academy mimi ndie nilikuwa nahodha,jambo ambalo halikuwa rahisi kwa raia asiekuwa mwenyeji,kwenye timu hio nilinyakuwa vikombe 2. Mwaka 2012 mwanzoni nika amuwa kurejea nyumbani Burundi ambapo hadi mdaa huu naendelesha safari yangu yakucheza mpira.
-AH: Twambie kuhusu kuingia kwako kwenye timu ya taifa ya Burundi ( Intamba Murugamba)?
*Mc Arthur : Duuh! Haikuwa rahisi na Warundi kila siku wanasema 'Ntawurya akatamugoye' namimi kila siku nawaza ushindi (Hasta la victoria siempre) ,safari ilikuwa ndefu ndugu.Mwaka 2007 nilioredheshwa dakika ya nyuma kwenye kikosi kilichodiriki kombe la CECAFA CHALLENGE CUP (Under 17),ila wakati huo bahati haikuwa yangu kwani makipa wawili Claude HARERIMANA a.k.a Massop na AMIDOU Hassan a.k.a AH walionyesha kiwango kizuri kunishinda kwa Mkufunzi Mmisri HUSSEIN Mahfouz . Kipindi ico nakumbuka Burundi ili shinda (win) kwa mara yake ya kwanza michuano hio yakikanda kuanzishwa. Sikuchoka nilizidisha juhudi na ilisalia kuwa kama ndoto vile kuichezea siku moja timu ya taifa , nafkiri kutokana na pafomansi (performance) nzuri nilio onyesha kwenye msimo uliopita kwani nakumbuka mwaka jana nilipotoka nchini South africa nilijiunga kwenye duru ya marudio na timu ya Lydia ludic Burundi Academie,apo niliwakuta magolikeeper wajuzi kama NYABENDA Athanase alias Cimba na Amidou Hassan alias AH wao wawili ndio walikuwa sambamba kwakuisadia club hio kuendelea kufanya vizuri kwenye msimamo wa ligi nchini. Mkufunzi Olivier NIYUNGEKO alias Mutombola alipenda nijiunge na timu yake namimi sikusita kwani ni timu iliokuwa na muonekano mzuri baada yakuonyesha kandanda safi kwa upande wa Kombe la Shirikisho barani africa (LLB Ac. 3-0,2-0 Atletico Semu ya Guinea Equatorial na 1-1,4-1 kufungwa zidi ya timu kutoka nchini Misri) Haikuniwea rahisi ila nilitumika vyakutosha hadi kusalia namba moja. Nilianza kuitishwa mara ya kwanza kwenye timu ya taifa na Coach Mmisri Nassim Lofti ilikuwa nikikosi cha wachezaji wanaochezea nyumbani kwenye match iliotupambanisha na kikosi cha vijana walio chini ya umri wa miaka 17 (-17) kutokea nchini Russia, kwenye pambano hilo sikucheza,match yangu ya kwanza niliocheza ilikuwa ni Uganda kwa upande wa mashindano yakikanda CECAFA CHALLENGE CUP, tilikuwa kwenye match yetu ya pili tukipambana na taifa Stars ya Tanzania,huo ndio ulikuwa mwanzo hadi mdaa nashkilia namba moja kwa magolikipa wa hapa nchini.
-AH: Kwani unafkiri unawazidi nini wengine?
*Mc Arthur: La ajabu hakuna bali,najikwauwa vyakutosha mazoezini na kila siku nawaza 'Hasta la victoria siempre',yaani ushindi na kuwa kwenye pafomansi nzuri. Nawashauri wenzangu watumike sana kwani kuwa kipa na ukiwa na mazoezi madogo haiwezi kuwa rahisi kuwa juu.
-AH: Kwani kwasasa uko mu timu gani?
*Mc Arthur: Nachezea kwenye timu ya Flambeau de l'Est,ni timu kutoka Mkoani Ruyigi,na tumesimama vizuri kwenye msimamo kwani hadi mdaa huu tuko wa kwanza,nani imani tutafika mbali kwani vijana wangu nawa amini sana.
-AH: Una ndoto gani?
*Mc Arthur: Nina ndoto yakuwa Mchezaji wakulipwa (professional player) kuichezea Club kubwa na yenye jina likubwa ulimwenguni.
-AH: Nashkuru sana,na kila la kheri na fanaka...
*Mc Arthur: Nashkuru pia AH kwa kazi yako,usichoki...
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire