Jana Jumaa-pili Tarafani Nyakabiga ndipo yalifanyika mashindano ya Primusic 2013 ngazi ya Robo fainali, mashindano hayo yaliwapambanisha wasanii 46 kutoka pande 4 za Burundi ,Mikoa yote ikiwa imewakilishwa . Jumla ya wasanii 12 ndio waliochaguliwa na Kamati inayo undwa na Wachakachuaji 5 pakiwemo BUDDY Magloire , ALIDA , ARNAUD , STEVEN SOGO na AMIR Pro walioteuliwa kwa uwaminifu na kampuni ya Brarudi kuja kukata mzizi wa fitna nakuwapa pointi wasanii waliopambana . Kazi haikuwa rahisi kwa upande wao kwani wasanii waliopambana walionyesha uwezo wa hali ya juu nakuimarisha wazi kuwa walikuwa wanahiaji sapoti kama hiyo ili waweze kuonyesha viwango vyao vyamuziki .
Burudani ilikuwa vile vile ni yakutosha kwa ma elfu na ma elfu ya raia kutoka pembe zote za Burundi waliohudhuria kushabikia wassanii wao waliokuwa mashindanoni . Kinyume na Sat B , Rally joe ambao ni wabalozi wa Primusic mwaka huu ,alikuwepo vile vile General FIZZO ,kiungo bora kati ya viungo ambavyo gwaride hii ya mziki nchini inavyohitaji ili Burundi ifike mbali zaidi . Raia walifurahi na walionyesha ushirikiano tosha kwa Wasanii hao walipokuwa wanaimba nyimbo zao uku wakizicheza na kuzi imba sambamba na wenyenazo . Walionekana vile vile kwenye jukwa MKOMBOZ na R Flow waliposhirikiana na Fizzo kwenye pini 'BAZA Rmx' . Jopo la watangazaji kutokea radio, Television na majarida mbali mbali walijifkia kushughudia nakuwea macho wale ambao hawakupata fursa yakujitokeza japo tamasha ilikuwa bure kwa upande wa kiingilio . Majina 12 yalitajwa na Jopo la wachakachuaji ( JURY) kwakutumia bahasha (Enveloppe) . Ilikuwa ni faraja kwa waliochaguliwa na fair play kwa walioshindwa na kuahidi kufanya vizuri mwakani kwani nikinukulu baadhi yao ' Haburana babiri hagatsindwa umwe '. Majina 12 yaliotajwa na jopo hilo ni pamoja na :
Pichani : 12 walioshinda. |
Georges Nahayo ( Bujumbura ) * Ni mtoto wa Babby John.
Irandagiye Aletta ( Mwaro )
Olga Ntaganzwa ( Kirundo )
Jean Marie Ninteretse ( Bujumbura )
Patient Matabaro ( Bujumbura )
Amissi Jean El Pedro ( Bujumbura )
Mugisha Jean junior ( Gitega )
Gateka Landry Michel ( Muyinga )
Mujimbere Gabriel ( Bubanza )
Bitariho Halidi ( Bujumbura )
Mfura Alain Michel ( Kirundo )
Duru ifwatayo ni nusu fainali imepangwa kufanyika siku ya Jumaa-mosi ijayo tarehe 1/September/2013 Mkoani Gitega kwenye uwanja wa mpira wa miguu , kati ya hao 12 watasalia 6 watakao pambana fainali tarehe 18/September Mjini Bujumbura...
Baadhi ya picha :
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire