dimanche 25 août 2013

CONFEDERATION CUP : ACADEMIE TCHIE 2 - 1 AC TANGANYIKA

AC TANGANYIKA
Mchuano wa pili wa nusu fainali kwenye kinyanganyiro cha kombe la Shirikisho ulifanyika leo kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore kati ya Academie Tchite na AC Tanganyika timu pekee ya daraja la pili iliobahatikiwa kufika kwenye ngazi hio mwaka huu. Bao la kwanza lilifungwa na Manishimwe Alain kwenye kipindi cha kwanza ilikuwa dakika ya 32 , bao lililo ingia kupitia mkwaju wa penali . Walipotoka mapumzikoni ndipo Manirakiza Cedric ali ipa ushindi timu yake dakika kama 15 za kipindi cha pili, palipo salia dakika 1 kipenge cha mwisho kipulizwe ndipo AC Tanganyika ilipata bao lakufutia machozi.Fainali itazipambanisha timu za LLB Academic na Academie Tchite ,zilipopambana kwenye Primus league ,duru ya awali Tchite ilwalazimisha kwa bao 2-1 . Ni naniatakae chukuwa  fainali nakujikatia tiketi yakushiriki kombe la shirikisho mwakani ? Wait & see...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire