lundi 20 mai 2013

UGANDA : TERRY WEST yuko anarikodi pini mpya na Washington...

Msanii chipukizi mwenye sauti nyororo ,sauti tamu anaekuja na kasi ya hali ya juu kwenye ulimwengu wa mziki nchini Burundi IRAKOZE Terry West , ni mmoja kati ya wanao unda kundi nzima la Question G (Josdy, Albi , Lil Soso...) toka tarehe 11/May auliziwa  Mjini Kampala / Uganda  akiwa amejielekeza  kwenye mpango mzima wakurikodi pini moja ao mbili chini ya ufundi wa Producer machachari nchini pale anae tambulika kwa jina la WASHINGTON . Producer huo aliwaweka juu vijana wawili Radio na Weasle toka kwenye kundi la GOOD LIFE . Msanii huo alilonga na blog yenu na akawa ametuwekea wazi kuwa :" Nimetulia nakula matoki Uganda , nimepelekwa na Mkubwa wangu flani anae kubali kazi zangu ili nirikodi pini moja ao mbili chini ya ufundi wa hali ya juu wa Best Producer toka pande za Kampala WASHINGTON , pini nitakayo achia hivi karibuni itasimama na jina *Niwewe* ." Aliongeza nakusema :" Hadi mdaa huu nimeshajaliwa kukutana nae,beat tumeitengeneza , sauti tayari nimeshaingiza toka siku ya Ijumaa tarehe 17/May kinachosalia niyeye kumalizia kuichanganya na kuichakachuwa (Mixage) kisha nitimbe Buja kuiwaskilizisha Washabiki wa miondoko ya burundi flava . Amekubali sauti yangu nakuniakikishia kuwa Burundi tunacho kipaji ila tunakosa watu wakutupa shavu ili kazi yetu ya mziki izidi kupiga atuwa zaidi pande zote kama wanavyotetemesha dunia alitaja KIDUM na wengineo tokea Burundi ." Ikumbukwe kwamba TERRY WEST amekuwa Msanii wa pili kwenye mwaka huu kutoka Burundi kutengenezewa pini na Producer huo...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire