lundi 16 septembre 2013

Dar es Salaam : Demunga afunga bao lake la kwanza,KAVUMBAGU kwenye orodha ya wafungaji bora,Simba na fasi ya pili kwenye msimamo...

Simba : Demunga na Tambwe mchezo wao wa pili wakiwa kwenye 11 wa mwanzo...
Wachezaji wa Burundi wazidi kunga'ara kwenye viwanja vya soka nchini Tanzania, kaze Gilbert na Tambwe Amissi baada yakusajiliwa na timu ya   SIMBA SC ,  huu ulikuwa ni mchuano wa pili wakiwa uwanjani  kinyume na mchuano wa kwanza waliokuwa waliziwilia kutokana na karatasi zakuwaruhusu  kucheza ,jumla ya michezo 3 ambayo tayari Simba ilishacheza  Tambwe hajaona lango kinyume na Kaze Gilbert ambae alipachika bao 1 kati ya 2 timu yake iliofunga kwenye mchuano wa juzi . Simba  wanaweza kupanda kileleni Jumatano wakiifunga Mgambo na JKT Ruvu wakafungwa na Ruvu Shooting .JKT Ruvu inaweza kusimamishwa na Ruvu Shooting Jumatano Mabatini- maana yake Simba SC ina nafasi ya kupanda kileleni kwa mara ya kwanza msimu huu ikiifunga Mgambo JKT kesho kutwa .

Didier Kavumbangu ana mabao mawili baada ya mechi tatu


Hakuna mchezaji aliyefunga zaidi ya mabao mawili hadi sasa na wachezaji sita Jerry Tegete, Didier Kavumbangu, wote wa Yanga SC, Jonas Mkude wa Simba SC, Elias Maguri wa Ruvu Shooting, Bakari Kondo wa JKT Ruvu na Saad Kipanga wa Rhino Rangers wamefungana kwa mabao mawili kila mmoja baada ya mechi tatu.
Kati ya hao ni Jonas Mkude pekee aliyefunga kwa penalti bao lake moja.
Ligi Kuu itaingia katika mzunguko wake wa nne keshokutwa, mabingwa watetezi, Yanga SC wakirejea Uwanja wa Sokoine, Mbeya kumenyana na Prisons.
Simba SC itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar itaikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Azam FC na Ashanti United Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Coastal Union na Rhino Rangers Uwanja wa Mkwakwani, Tanga,Mtibwa Sugar na Mbeya City.Uwanja wa Manungu, Morogoro na Ruvu Shootings dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Mabatini, Pwani.Msimamo,wiki ya 3
1JKT Ruvu33006069
2Simba SC32105237
3Ruvu Shooting32015236
4Yanga SC31207345
5Azam FC31207345
6Coastal Union31203125
7Mbeya City31203215
8Mtibwa Sugar311123-14
9JKT Mgambo310213-23
10Kagera Sugar302112-12
11Rhino Rangers302135-22
12JKT Oljoro301214-31
13Tanzania Prisons301206-61
14Ashanti United300317-60


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire