vendredi 30 août 2013

Burundi Movies : Filamu * Mwanzo wa Mwisho * hivi karibuni madukani



Muigizaji Mrundi ambae kwa muda huu anaishi nchini Holland ameachia kipande cha filamu yake inayosimama na jina la * Mwanzo wa mwisho * kwenye ukurasa wa kijamii Youtube (  http://www.youtube.com/watch?v=zragZ1utqNw ) . SALLAI MAJASIRI tulipohojiana nae alifunguka nakusema haya :" Hii ni Filamu yangu ya kwanza ambayo nimetengeneza, imetokana na maisha ya sasa kipindi hiki kinacho onekana ni kipindi cha mwisho kutokana na dalili nyingi zilizotajwa kwenye biblia kuonekana kipindi hiki. Nili igiza na mdogo wangu mpendwa Gilbert ,akiwa kinara wa filamu hii , akifuatiwa na Sandrine, Jarno ,Blandine, Antoinette ,Solange , Kuba , Gabriel , Sandrine , Betty, Solange, Leyla . Mwanzo wa mwisho ni filamu inayozungumzia vituko vinavyofanyika ndani ya kanisa nyakati hizi zinazo sadikika kua ni za mwisho kwa maana kwamba Yesu Yu karibu kuja . Inagusia maisha ya wachungaji wawili, mchungaji wa ukweli na wa uongo. Yule mchungaji wa ukweli alikuwa akihubiri juu ya kuja kwa Yesu na utakatifu na Yule mchungaji wa uongo, alikuwa akitumia kanisa kujitajirisha . Inagusia pia, maisha ya ndoa . Tunapata kuona jinsi msichana mmoja kutoka Africa, Alioleka Netherlands, kisha akabadilika na kuwa na tabia mbovu mara tu alipojiunga na marafiki wanafiki. Akaaanza kumdharau mumewe na kulewa, kurudi nyumbani amechelewa . Mwishowe, Yesu anaporudi, wachache wananyakuliwa, na wale walioishi kinyume na neon la Mungu, wanaachwa nyuma wakilia . " Hii apa ni kwa niaba ya waumini wa dini ya kikristo...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire