mercredi 24 juillet 2013

Intamba Murugamba : Orodha ya Wachezaji 18 waliojielekeza Sudan kwenye mchuano wa marudio Mjini Kharthoum

Intamba,11 walio anza mchuano wa awali.
Leo hii Jumaa-tano saa tatu asubuhi ndipo kikosi cha timu ya taifa ya Burundi "Intamba Murugamba" kinasafiri kuelekea nchini Sudan ya kaskazini kuchuana mchuano wa marudiano na kikosi cha "Mamba wa Nil" ifakapo Jumaa-pili tarehe 29/July/2013 insha'allah. Kinyume na Jopo nzima ilio undwa na Wakufunzi wawili ( Nassim Lofti na Niyonkuru Amars) na Mganga umoja,muwakilishi wa Shirikisho la Soka nchini (FFB),muwakilishi wa Wizara ya michezo vijana na utamaduni,ambae anasimamia msafara na Mtangazaji,ipo orodha ya Wachezaji 18 ya Wachezaji ambao wamejielekeza kwa hari na nguvu ya hali juu kuiwakilisha nchi yao kwenye mchuano huo wakihistoria pande zote mbili kwani hakuna toka michuano ya CHAN kuanza nchi hizo mbili kuwakilishwa. Jana usiku nilipata fursa yakuhojiana na baadhi ya Wachezaji wakaniwekea wazi kuwae .
-
 Tambwe Amissi :" Kwa ujumla tupo fity,na Mungu akipenda lazima tuiandikishe nchi yetu kwenye historia ya mpira baada yakutwa kombe kwa mara ya kwanza ya CECAFA kwa upande wa klabu ,na uko tunapo elekea nina imani kuwa tutafanya vizuri tena akipenda Mungu."

- Issa Hakizimana :" Insha'allah lazima tuwa ayibishe kwao".

- Lucio :" Kubushobozi bw'imana tuzobatsindirira iwabo,ntankeka kuko twaragize imyimenyerezo ikwiye kandi ishimishije." akimaanisha :" Kwa nguvu za Mungu tutawafungia kwao,bila shaka kwani tulijianda vyakutosha tena mazoezi tulioyafanya yanaridhisha mno."
Sudan ,11 walio anza mchuano wa awali .

ORODHA YA WACHEZAJI 18


(1)ARAKAZA Mc Arthur . (3) Rashid Léon , (17) Hakizimana Hassan L'Homme(C),(15) Kaze Gilbert , (14) Issa Hakizimana , (6) Nduwarugira Christophe, (10) Shassir , (2)Duhayindavyi Gael , Célestin Habonimana , (11) Aime Nzohabonayo , (9) Tambwe Amissi.(18)Rugumandiye Yvan , (8) Nkurikiye Leopold Kaya , (5) Nsabiyumva Frederick , (16) Ndayishimiye Christophe ,(7) Nahimana Claude , Ndikumana Yussuf Lule (LLB),Shabani Tchabalala.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire